2017-01-09 16:18:00

Kard.Jean-Pierre Kutwa:Asema vurugu zimetawala sana Pwani ya Pembe


Machafuko ya kisiasa yamerejea tena nchini Pwani ya Pembe baada ya  wanajeshi kufyatua risasi hovyo katika baadhi ya miji   ya nchi ikiwa pamoja na mji Mkuu Abdjan ambapo uasi ulianza kwa upande wa Bouaké,ambayo ndiyo ngome ya uasi iliyokuwa imegawanya nchi kati ya mwaka 2002 na 2011 na ngome hiyo ndiyo ulikuwa msingi wa uchaguzi wa Rais wa sasa Alassane Ouattar. Makubaliano ya maaskari  hao yalikuwa  na Waziri wa Ulinzi Alain Richard Donwahi aliyekuwa amekwenda tarehe 7 Januari 2017 huko Bouake.Makubaliano hayo yalikuwa ni kuongeza mishahara , kulipa malipo ya nyuma ya mishahara , na kufanya utaratibu wa haraka wa matangazo ya kuongeza vyeo.

Uasi wa kijeshi kwa mwaka huu ulikuwa umetanguliwa na ule wa 2014 ambao pia walikuwa na lengo la madai ya kiuchumi.“Nchi ya Ivory Coast ina mgogoro mkubwa mwaka kuanzia  mwaka 2002 -2011 ambapo ulisababishwa na mgawanyo wa nchi sehemu mbili ya kwanza ya serikali tawala na sehemu nyingine iliyokuwa imechukuliwa na waasi.Mgogoro huo ni ishara za makovu makubwa katika jamiii mahalia.”Huo ni ujumbe wa Kardinali wa nchi ya Ivory Coast.

Katika ujumbe wake wa kufunga  mwaka 2016  Kardinali Jean-Pierre Kutwa, Askofu Mkuu wa Abidjan, alikumbuka hali ya vurugu zinazaojitokeza katika jamii ya Ivory Coast: na kusema " kama mnavyoona hawa vijana na watoto daima wanaishi katika vurugu zinazozaliana kila sehemu kwani: vurugu shuleni , vurugu katika siasa, vurugu ndani ya familia, vurugu kwenye skrini ya televisheni, vurugu katika michezo  ya kisasa ambayo sisi watu wazima tunawapatia.” 

Akikumbuka vijana wanaojaribu kukimbia na kuhama nchi kwenda nchi nyingine , Kardinali Kutwa  alisistiza kuwa hata hii inaweza kuwa aina ya vurugu na unyanyasaji na kwamba unazidi kupanuka ambapo hatuna budi ya kutafuta ufumbuzi wa haraka iwezekanavyo”
Kwa mujibu wa Kardinali anasema ibabidi kujiuliza sababu zinazo wasukuma vijana kuacha, nchi yao na kwenda nchi nyingine na kuuliza” mazingira yetu, hali ya ndani kiuchumi, ajira , masoko kwaajili ya maisha endelevu vinaweza kuwa motisha wa kuweka mwisho wa mfasara huo kwa nyakati mpya?au  Je, tunawezaje kuelewa ukweli kwamba watoto wetu wanao wasiwasi wa kupata fedha za haraka iwezekanavyo bila juhudi na kutokwa jasho? Je ina maana gani kwao utamaduni wa sifa?

Sr Angela Rwezaula.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.