2017-01-08 10:18:00

Askofu Giza Antonious asema Misri siyo kama ilivyokuwa mwanzo


Tarehe 7 Januari 2017 ilikuwa ni sikukuu ya kuzaliwa kwa Bwana  kwa makanisa yanayofuata kalenda ya Juliani. Kama  alivyokumbuka  baba Mtakatifu Francisko wakati wa sala ya malaika wa Bwana tarehe 6 Januari 2017,  ya kwamba Makanisa ya Mashariki yanayofuata Kalenda ya Juliani , walikuwa wakijiandaa kuadhimisha sikukuu ya kuzaliwa kwa Bwana tarehe 7 Januari.


 Lakini ni makanisa yanayopatwa  mashambulizi ya kigaidi na majeshi ya kijihadi.Pamoja na hayo yote wakristo wa maeneo hayo hawakukosa kusheherekea siku ya kuzaliwa kwa Bwana , kama vile Wakoptiki wa Misri.
Ili kupata namna walivyokuwa na maandalizi hayo, kabla ya sikukuu yenyewe kuanza, mwandishi wa Habari wa Radio Vatican alifanya mahojiano kwa simu  na Askofu Giza Antonious Azizi Mina akisema kwamba, wanaishi hivyo katika hali ya ushuhuda wa Kanisa wakimsubiri Bwana kwaajili ya wokovu wao.

“Kila kitu kinaendelea kwa utulivu  japokuwa ni  ule uchungu na huzuni kutokana na wakristo wao 25 waliopoteza maisha katika shambulizi lililotokea la Kanisa kuu la Mjini Cairo tarehe 11 Desemba 2016. Hata Hivyo Askofu Azizi anasema kwa hali ya Misri kwa upande wa ngazi za kisiasa kuwa, “kwa bahati mbaya kutokana na fikra za kipumbavu za hao magaidi, zimesababisha jamii kutokufikiria kwa namna moja, kwasababu wote wasio fikiria kama wao wanaonekana maadui”. “Hata hivyo vituko vya kutishia kwa upande wa Misri, kwa sasa vinapungua nguvu yake  kwani siyo kama mwanzo, japokuwa fikra zinazotawala daima ni hizo tu kwasababu, ni miaka 30, 40 labda na zaidi , wameendelea kupandikiza mbegu za  mawazo yao, mawazo yao finyu, kwani ni kushikilia tu kile wanachokiona wao , bila kuacha nafasi ya maoni ya mtu mwingine”.

Na kwa upande wa majadiliano  ya maisha kati ya wakristo  na waislam wa Misri, Askofu anasema , mazungmzo yanaendelea mbele , na hasa  kwa upande wa watu  walio wazi: wako karibu na wanasaidiana kati yao , lakini wapo hata wengine ambao hawaonekani , na siyo kwa upande wa wakristo na kwa waislam bali katika ngazi ya kibinadamu, kwa mfano hata ndugu kwa ndugu. Hakuna hule upendo ulio kuwapo kati yao wamisri wa zamani ,maana  kwa sasa upo hata uwezekano wa ndugu kumpeleka ndugu yake wa damu mahakamani kwa kosa tu la kiupuuzi.


Halikadhalika aliendelea kueleza jinsi  jamii ya Misri imebadilika , akitoa mfano kwamba ;vijana wao walikuwa na tabia ya kupendana wao kwa wao,kuupenda  utamaduni wao wa kuishi kwa pamoja , wakipokeana, kukaribishana na walikuwa wako wazi, bila kujifunga wao kwa wao,hata kama ingekuwa ni kufia kwa ajili ya haki ya mtu mwingine  na hata kama ingekuwa ni kumgharimia mwingine, la muhimu ilikuwa ni kuendelea mbele.

 

Aidha akieleza  nini sasa maana ya krismasi iwapo mantiki hiyo kwa sasa ni ugumu kwa upande wa Misri na kusema; ” inabidi wasiwe na chuki, kwasababu ikiwa watafikia hatua ya kuchukia ni kusema kwamba wameshindwa". "Hiyo ni kwasababu ujumbe wa Krismasi ni wa upendo na amani.Hawali ya yote tunapaswa kuwa na amani ndani ya roho zetu ili baadaye kuwapelekea amani wengine, na wakati huo huo tunapaswa kuwaombea wote, hata wale wanaotuchukia na kutushambuliwa hata kama hawataki  kuona nyuso zetu ; tunapaswa kuwapa ushuhuda wa upendo ili kusheherekea kweli sikukuu ya kuzaliwa kwa Bwana”.


Pamoja na kusema kutoa ushuhuda huo, Askofu alielezea juu ya maisha ya Misri leo hii yaliyo magumu, na kusema “siyo tu kwa wakristo peke yake bali ni kwa wakazi wote wa Misri.Maadili yamebadilikia, hakuna tena thamani ya upendo, bali kinachotawala ni ubinafsi.
Tunapaswa kuanza kwa upya”, alisisitiza,  na kumalizia akisema  "msitusahahu katika sala zenu , kwani tunahitaji msaada wa sala zenu!.Tunatambua vema nguvu ya sala ambzao utufanya tubaki kidete katika upendo wa Mungu: na hiyo ndiyo itakayotukomboa.

 

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.