Askofu mteule João Carlos Hatoa Nunes wa Jimbo Katoliki Chimoio ametoa wito wa ujenzi na udumishaji amani wakati akihojiana na mwakilishi wa Radio Vatican mjini Maputo Hermínio José kwamba, ni kuhakikisha amani katika nchi kama ilivyotangazwa na vyama vyote viwili , chama cha Serikali FRELIMO na cha upinzani RENAMO. Askofu litoa wito kwa vyama vyote viwili vya kisiasa kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha kwamba amani inapewa kipaumbele cha kwanza kitaifa, kwani amani ni jina jipya la maendeleo endelevu ya watu!
Askofu João Carlos alisema Frelimo na Renamo wanahitaji kusikiliza kilio cha
watu walio na kiu ya amani na alisisitiza kuwa watendaji wote wa sera za kisiasa
katika mchakato wa Amani,wanapaswa kuwajibika.Kuna haja ya kufanya kile kinachowezekana
kwaajili ya kutafuta Amani ya kudumu.
Muda mfupi baada ya Krismasi, Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi alinukuliwa na Radio ya
Msumbiji akisema kuwa "kuna kila sababu ya kuwa na matumaini kwamba amani na ufanisi
inaweza kufikiwa mwaka 2017".
Rais Nyusi alibaini kwamba Kiongozi wa upinzani wa RENAMO , Afonso Dhlakama alimpigia
simu , na wote wawili walipata muda mrefu wa mazungumzo ya simu yaliyokuwa ni yenye
manufaa.Kiongozi huyo wa Taifa la Msumbiji alionyesha utashi wa wazi wa kuwa na
mazungumzo ya kisiasa na Dhlakama.
Dhlakama alitangaza kuongeza muda wa kusitisha mapigano ya muda mfupi wa chama chake
4 Machi 2017. Katika mkutano na wanahabari, Jumatatu 2 Januari 2017 , Dhlakama alionyesha
kuridhika kutokana na uhakika kutoka kwa Rais Nyusi kwamba vikosi vya usalama wa
serikali watajiepusha na kushambulia RENAMO na kuacha utekaji nyara wa wanachama
na wajumbe wake. Katika ujumbe wa Siku ya 50 ya Kuombea Amani Duniani kwa mwaka 2017
Baba Mtakatifu Francisko ametoa wito wa kurudia upya utamaduni wa kutokutumia nguvu,
na kuujulisha ulimwengu na wadau wa siasa za kimataifa kwamba majibu ya migogoro
kwa njia ya vita ni kuzaa vurugu zaidi.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |