2017-01-05 13:01:00

Misri :Katika maandalizi ya Vijilia ya Noel yaanza na damu


Mwananchi wa Misri  na mkristo wa kikoptiki aliuwawa kinyama  huko Alessandria Misri tarehe 3 Januari 2017  na kijana mmoja akitoa sauti ya “Allahu Akbar”.
Hayo yalisemwa na Televisheni ya Al-Arabiya, na muuaji huyo alipatikana na kukamatwa ndani ya  masaa 24 kutokana na mitambo ya ulinzi ya kupiga picha iliyowekwa  katika maduka mbalimbali.

Kupatikana kwake ilitokana na  picha zilizoonesha tendo la muuaji kumfikia mtu akiwa amekaa na kuchomoa kisu mfukoni na kumkata shingo na baaaye mtu huyo kutoroka.

Hili tukio limejitokeza wakati  Jumuiya  ya Kikoptiki ya huko Alessandria wanajiandaa kusheherekea sikukuu ya kuzaliwa kwa Bwana ikiwa ni  liturjia ya Kiotodosi, itakayofanyika tarehe 7 Januari 2017,  na tukio hilo limeaacha watu bumbuazi.
Wakati wakitafuta mwelekeo  wa kisiasa wa huyo muuaji,wapelelezi  wanafikiri  labda ni kwasababu ya kuuza vinywaji vya kulevya  katika duka la huyo mtu aliye uwawa kinyama .

 








All the contents on this site are copyrighted ©.