2017-01-04 15:51:00

LIBYA: WHO kusambaza dawa za virusi vya ukimwi Benghazi


Shirika la Afya duniani, WHO limesema kiwango cha maambukizi ya virusi vya Ukimwi huko Benghazi, nchini Libya kimeongezeka tangu kuanza kusambaaa  mwaka 2011.Tathmini ya shirika hilo imeonyesha kuwa hali hiyo imesababishwa na kuporomoka kwa mfumo wa afya nchini humo ikiwemo mfumo wa upataji na usambazaji wa dawa.Tayari Wizara ya Afya ya Libya imeomba WHO isaidie kupatikana na usambazaji wa dawa hizo kwani ukosefu wake unatishia uhai wa watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi.

Taarifa ya  umma imeripotiwa kutaka hatua ya haraka kwa kuzingatia kuwa mwaka 2016 pekee watu 6330 nchini Libya walisajiliwa kuwa na virusi vya ukimwi.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radi Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.