2017-01-04 15:34:00

Kard. Gracias asema kutokutumia nguvu ni kuleta haki na amani


Ukosefu wa roho ya asia ni kutumia nguvu: hayo ni maneno yaliyosemwa na Kardinali Oswald Gracias, Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Mumbai ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Asia (Fabc). Akitafakari juu maadhimisho ya siku ya 50 ya kuombea amani kwa mwaka 2017 yaliyoongozwa  na kauli mbiu ”Kutokutumia nguvu: mtindo wa siasa ya amani”. Kardinali huyo alidhibitisha akisema ipo mifano halisi ya wasisi barani Asia ambapo hawakutumia nguvu kama vile Mahatma Gandhi muasisi wa taifa la India na Mama Theresa wa Calcutta, shuhuda wa upendo na huruma ya Mungu.

Kutokutomia nguvu aliendelea Kardinali Gracias , siyo kwamba ni ukosefu wa nguvu bali ni roho ya amani, msamaha , uwelewa na kupokea.Tunu hizi msingi zinatupelelekea ujenzi wa amani ndiyo  msingi na muhimu wa roho ya kutokutumia nguvu, ambayo inatufanya tuunde jamii ambayo wote wanaweza kuheshimiana, kuwa na haki, amani na haki za binadamu wote ,na hata  kwa wale waliobaguliwa. Katika nyakati zetu , jamii nyingi zimejikuta zimeangukia katika mkumbo wa utandawazi na huo unaongaza nchi na kuifanya misingi ya kwanza iwe mbali na upeo wa amani na  maelewano,na pia hali ya kuwa pamoja kama Ghandi alivyopigania na kwamba alivyokuwa ameijenga nchi yetu pendelevu.

Akimtazama pia Mtakatifu Mama Theresa wa Calcutta, Kardinali alisema” ni ishala na mfano wa nyakati zetu, kwani ni utume usio na mwisho unatoa shuhuda wa  upendo wa Kristo , zaidi ya mipaka ya kidini , utamaduni na kushinda utofauti wa lugha au mipaka, aliongeza kardinali wa Mombai Mtakatifu wa Calcutta ni mfano wa  kuigwa, na pia anatupatia changamaoto katika  ulimwengu ili ufanye chochote kwaajili ya wale wanaoishi pembezoni wamebeguliwa, na  kwa njia hiyo ni kuunda jamii ya kibinadamu na ndugu. Na mwishoni  Kardinali aliwataka wawe na roho hiyo ya kutokutumia nguvu ili waweze  kutatua migogoro na kupata  ufumbuzi wa amani na hasa katika kipindi hiki ambacho  mataifa  ulimwenguni yana endelea kukabiliana na migogoro ya kigaidi na kutumia nguvu.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.