2017-01-03 14:19:00

Pambaneni kwa dhati na biashara haramu ya binadamu!


Kila dakika mbili katika dunia , mtoto mmoja anaathirika na utalii wa ngono duniani. huu ni mtandao wa biashara haramu ya binadamu; Ni zaidi ya milioni 200 ya watoto wadogo na kati ya 73 milioni ni wale ambao hawajafikia miaka 10 kulazimika kufanya kazi za kulazimishwa na  kila mwaka wanakufa 22.000 kwaajali.Kwa miaka 30 iliyopita inahesabiwa milioni 30 wameathirika na biashara haramu ya binadamu! Ni hali ya kutisha ambayo ndiyo lengo hasa la kufanya siku ya sala ya kimataifa  kwaajili ya  kukomesha  biashara hiyo  haramu ya utumwa , ambayo inafikia kilele chache 8 Februari 2017 ikiwa ni  mwaka wa tatu kufanyik na  itakayoongozwa na kaulimbiu  “hawa ni watoto na siyo watumwa”

Kutokana na tukio hilo , Baraza la Maaskofu Katoliki wa Ufaransa , wametoa wito kwa Serikali , kushughulikia mpango wa kitaifa juu ya kupambana na biashara haramu ya binadamu  na hasa wa watoto.Ujumbe huo umetangazwa kupitia mtandao wa Baraza la Maaskofu uliotiwa sahini na Askofu Jacques Blaquart, wa Jimbo la  Orléans na Rais wa Baraza kwaajili ya mshikamo. Ujumbe huo una lengo la kuhamasisha jamii yote  juu ya matukio haya ya utandawazi licha ya wajibikaji  wa kila Taifa.Kwenye ujumbe huo , unasema biashara ya binadamu kiukweli bado hautambulikani na kwamba inafikiriwa kana kwamba ni jambo la wakati uliopita au jambo hili lipo lakini liko katika nchi zilizo mbali na katika mabara mengine.

Lakini kinyume chake, leo hii biashara hii inasasababishwa na mambo mengi ambayo aliyataja na kusema kama “ kipeo cha nchi katika  uchumi, migogoro, majanga ya asili, uhamiaji wa kutaka au kulazimika kwa watu. Na cha kutisha zaidi ni  juu ya unyonyaji wa  utalii wa ngono na kazi za kushurutisha majumbani, ndoa za kulazimisha , wizi, mauaji ya kutumia silaha, biashara ya viungo na watoto kuwa maaskari.Halikadhalika ujumbe unataja aina nyingine zinajitokeza kama vile ongezeko la vitendo vya  kigaidi ni kwasababu , wanyonyaji wanatambua namna ya kupata faida  kupitia njia za  utandawazi hasa kulenga katika  katika udhaifu unaosabishwa  kushuka kwa maendelo ya kiuchumi, kijamii, kisiasa na mabadiliko ya hali ya hewa.

Waathirika daima wanadanganywa , wanatekwa , wanauzwa , wanalazimishwa kwa nguvu kimwili, kiakili na kisaikolijia .na hivyo Askofu Balquart anaendelea kusema “ tunahesabu ni watoto wengi , kama ilivyo kwa  wahamiaji ambao ndio wamekuwa midomoni mwa utumwa.Hiyo pia ni kutokana na kuingia nchini bila ruhusa,hujificha chini ya watu hawa magaidi, bila ya kutambua ya kwamba hata bila ya kuwa na vitambulisho wanayo haki. Kinachotakiwa kwa sasa ni sera za kisiasa za kweli , ambazo zinaweza kupambana dhidi ya uharamia kwa kutumia vyombo maalumu vya kijamii.na hasa kwa kuwapatia Mahali pa kulala, chakula, afya na kuwakaribisha, kuwapa mafunzo ya kitaalamu , kuwasindikiza ili watambue  sheria na haki zao , zaidi hawa  waathirika wa biashara ya haramu  watoto wadogo amabao ni wahamiaji na wakimbizi wanaopaswa kulindwa dhidi ya  aina zozote zinazowakabili.

Siku ya kimataifa ya kupambana na bishara haramu ya binadamu  ilitangazwa  na Baraza la Kipapa la haki na amani ili kusali kwa pamoja na kutafakari juu ya biashara haramu ya binadamu, kufanyika kila tarehe 8 Februari ya kila mwaka, siku hiyo inakwenda sambamba na liturjia ya kumbukumbu ya Mtakatifu Josephine Bhakita kutoka Sudan, akiwa na miaka 9 alitekwa na kupelekwa utumwani ,ambaye baadaye akawa mtawa wa Shirika la Wakanosa. Ma kwa naana hiyo ujumbe huo unatoa pongezi ukisema "Tangu Baba Mtaktifu Francisko achaguliwe kuwa Papa mwaka 2013 ameendelea kuwachangamotisha waamini ili kupambana na donda hili ndugu linaloathiri utu na heshima ya binadamu!

Sr Angela Rwezaula 

Idhaa ya Kiswahili ya Radi Vatican.

 

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.