2017-01-02 10:20:00

Askofu Msaidizi Joào Nunes ateuliwa kuwa Askofu Jimbo Chimoio


Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi lililowasilishwa kwake na Askofu Francisco Joào Silota, M. Afr., wa Jimbo Katoliki Chimoio la kung’atuka kutoka madarakani. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu amemteua Askofu msaidizi Joào Hatoa Nunes wa Jimbo kuu la Maputo, Msumbiji kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki Chimoio.

Askofu Joào Hatoa Nunes alizaliwa tarehe 8 Machi 1968 huko Beira, Msumbiji. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, kunako tarehe 17 Julai 1995 akapewa daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 25 Mei 2011, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo kuu la Maputo na kuwekwa wakfu tarehe 10 Julai 2011. Tarehe 14 Januari 2012 akateuliwa kuwa ni Msimamizi wa kitume Jimbo Katoliki Beira na kung’atuka rasmi hapo tarehe 29 Juni 2012.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.