2017-01-02 14:52:00

António Guterres mwaka 2017 uwe wenye nuru na utatuzi wa migogoro katika sayari


Katika Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ambaye alianza  kazi rasmi tarehe 1 januari 2017, alitaka dunia kuungana naye katika kusaka suluhu ya matatizo lukuki yanayoikabili sayari hiyo.
Guterres ambaye  alianza rasmi jukumu lake hilo, alisema hayo katika ujumbe  wake wa amani kwa jumuiya ya kimataifa akisema mwaka wa 2017 uwe wenye nuru na utatuzi akisisitiza; "Katika siku hii ya mwaka mpya, nawasihi nyote muungane nami kuweka azimio la pamoja la mwaka mpya: Hebu na tuazimie kuweka mbele amani. Hebu na tuufanye mwaka 2017, uwe mwaka ambao kwao sisi sote, raia, serikali, viongozi tunahangaika kumaliza tofauti zetu.


Kuhusu madhila ya vita na athari zake Katibu Mkuu alisema hakuna mshindi zaidi ya mateso kwa raia kwani ; "Makombora mazito yanaangukia raia. Wanawake, watoto na wanaume wanauawa na wanajeruhiwa, wakilazimika kukimbia makwao, bila mali zao na kusalia hohehahe. Hata hospitali na misafara inalengwa."


 Hali kadhalika alizungumzia umuhimu wa mshikamano katika kufikia suluhu na kusema  "Kuanzia mshikamano na upendo kwenye maisha yetu ya kila siku hadi mazungumzo na kuheshimiana katika migawanyiko yetu ya kisiasa….Kuanzia kusitisha mapigano kwenye maeneo ya vita hadi kulegeza misimamo kwenye meza za mazungumzo na kufikia suluhu ya kisiasa.Amani lazima iwe lengo na mwongozo wetu."

Na Idhaa ya Radio ya UM

 








All the contents on this site are copyrighted ©.