2017-01-01 14:34:00

Papa Francisko: wasaidieni vijana kutimiza ndoto ya maisha yao!


Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi, tarehe 31 Desemba 2016 aliongoza masifu ya jioni kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, ikiwa ni maadhimisho ya mkesha wa sikukuu ya Bikira Maria Mama wa Mungu inayo adhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe 1 Januari na ni  sikukuu inayokwenda sambamba na siku ya kuombea amani duniani. Ndani ya masifu kulikuwa na Ibada ya kuabudu Ekaristi Takatifu, ambayo ilifuatiwa kama utamaduni wa Kanisa wimbo wa shukrani “Te Deum” kwa Mungu kwa kufunga mwaka wa kawaida na kuufungua mwaka mpya . “Kijibidisha ili vijana wapate kuwa viongozi wanaojishughulisha katika jamii yetu,na  ili waweze kupata   kazi yenye utu, pamoja na kushinda mantiki zinazomfanya kubagua wengine, ni wito wa nguvu uliochukua uzito mkubwa katika mahubiri yake.

Mara baada ya maadhimisho hayo, Baba Mtakatifu alisimama kidogo kusalimiana na Mstahiki Meya wa wa mji wa Roma Bi Virginia Raggi aliyekuwapo katika maadhimisho hayo. Halikadhalika  akiwa anaelekea uwanja wa mtakatifu Petro kuangalia Pango la Noeli alipokelewa na umati mkubwa wa waamini na mahujaji waliokuwa wamefurika kwenye viunga vya Kanisa kuu la Mtakatifu Petro kwa  shangwe; alipata nafasi ya alisimama mbele ya Pango na kusali kidogo kwa ukimya.

Baba Mtakatifu katika mahubiri yake katika mkesha wa Siku kuu ya Bikira Maria Mama wa Mungu, alianza na barua ya Mtaktifu Paulo kwa wagalatia; “Lakini wakati ule maalumu ulipotimia , Mungu alituma Mwanae aliyezaliwa na mwanamke akaishi chini ya sheria apate kuwakomboa wale walikuwa chini ya sheria ili sisi tufanywe wana wa Mungu”. (Gal 4,4-5). Maneno hayo ya Mtakatifu Paulo yanatufanya tutafakarin ni kwa ufupi lakini yanatoa utangulizi wa  Mpango wa Mungu kwetu sisi, tunaoishi  kama watoto . Historia nzima ya Uwokovu , inapata sauti kutoka kwa yule ambaye hakuwa katika sheria iliyokuwa imepangwa bali kwa  upendo,alikubali kuupoteza ukuu wake , ili apate kuingia kwa kupitia sehemu ambayo hakuna aliyekuwa anategemea apate  kutuokoa  sisi tuliyo kuwa chini ya sheria. Ndiyo habari mpya aliyo amua kufanya ya kuwa  mdogo na mdhaifu  kama kitoto kichanga, alimua kutukaribia sisi wenyewe kwa njia ya  mwili wake alitukumbatia  sisi mwili wetu, kwa udhaifu wake, akatukumbatia  udhaifu wetu , kwa udogo wake ,akatufunika udogo wetu

.Kwa njia ya Kristo , Mungu  hakujificha nyuma ya binadamu, bali alijifanya binadamu na kutushirikisha hali yetu.Hakukaa mbali na kujifungia fikra mwenyewe , bali yeye alitaka kuwa karibu na wale wote wanaojisikia kupotea, kulaumiwa, walioathirika, waliokata tamaa, wasiokuwa na kitulizo na  wenye hofu.Baba Mtakatifu aliendelea na mahubiri yake; Alitaka kuwa karibu na wote ambao wanajisikia  miili yao kubeba mzigo na kupotea  pia  ni wapweke, ili kwamba dhambi, aibu, majeraha, kukata tamaa na kubaguliwa ,  vitu hivyo visiwe na ushindi katika maisha yao.

Baba Mataltifu Francisko aliendelea kusema,  Pango la kuzaliwa kwa Bwana,  linatualika  tuwe na  mantiki hii  ya mungu. Mantiki isiyokazia upendelevu, juu ya ruhusa juu ya  kufanikiwa , bali ni matiki ya kukutana, ya kukaribia na kuwa karibuna wengine . Pango linatualika kuhachana na mantiki ya kupendelea na  kutaka kuwa juu zaidi ya wengine. Mungu mwenyewe amekuja kwaajili ya kuvunja minyororo hiyo ya upendeleo  unao sababisha  ubaguzi, na hivyo Baba Mtakatifu anasema   muwe  karibu kwa huruma ambayo inakataa  ubaguzi , na kuwafanya  kila kila mmoja awe na utu wake alio umbwa nao.Mtoto aliyevalishwa anaonesha , ukuu wa Mungu na kutufanya tutambue  wito wa zawadi  kama sadaka ,vilevile  ni kama chachu na pia  fursa ili kuunda utamaduni wa makutano alisisitiza Baba Mtakatifu.

“Hatuwezi kuruhusu tuwe wajinga.Tunatambua kwamba baadhi ya sehemu tumekuwa tukiishi kwa mantiki hii  ambayo utenga kwa kutenganisha,  ubagua kwa kujibagua , inafunga , tukifunga ndoto , na maisha ya ndugu zetu. Mbele ya Mtoto Yesu leo anataka  kuonesha  jinsi tulivyo na mahitaji ya Bwana, atuangazie kwasababu ni mara nyingi tuna ukosefu wa kuona ,na kubaki  kama wafungwa , na hiyo ni kwasababu tunataka tubaki katika mtazamo wetu na kulazimisha wengine kwa nguvu wafuate utaratibu wetu,kwa namna hiyo tunahitaji mwanga huu, ambao utufanye tujifunze  kutokana na makosa yetu ili tupate kuwa na madalilijo na kushinda. Alisistiza tena Baba Mtakatifu; Tunahitaji Mwanga huu unaotoka kwa yule  mnyenyekevu, na mjasiri anayetambua ni nani anatafuta kwa nguvu kuamka maramoja anapoanguka na kuanza upya.

Papa aliendelea kukazia akisema; tunapokaribia mwaka kuisha ,  tupo mbele ya pango kwaajili kutoa shukrani ambayo ni  ishala za ukarimu wake kwa maisha yetu na katika historia uliojionesha kwa namna nyingi katika udhuhuda wa sura nyingi zisizo tambuliwa na hata ambao wamehatarisha  maisha yao. Pamoja na hayo si kwamaba hawakuleta matunda au kufanya kumbukumbu ya wakati uliopita, bali tunafanya kumbukumbu hai amabayo kuwa na mwamko binafsi na katika jami kwasababu Mungu yupo pamoja na nasi.

Tukae mbele ya Pango kwa kutafakari Mungu pamoja nasi,  Mungu amekuwa nasi kwa kipindi chote cha mwaka  kutukumbusha kwamba kwa kila kipindi, kila wakati yeye ni mtoaji wa neema na baraka.Pango hilo linatupatia changamoto, ya kwamba hatutoi kitu, lakini hakuna yoyote aliyepotea. Kuangalia Pango hili ni kupata nguvu ya kutafuta nafasi katika historia bila kulalamika na kujibagua , bila kijifunga au kuvamia , bila kutafuta njia za mikato yenye kutunufaisha. Kutazama pango ni kutaka kutambua  ya kwamba muda tunao usubiri unahitaji mwamko na matumaini, na siyo ule wa kujikana kwa kutafuta madaraka  au mapambano yasiyo mwisho ya kutaka uonekane. Kutazama Pango ni kugundua Mungu anavyo tuhamasisha , ili tuwe sehemu yake ya utendaji , na anatualika  kuupokea kwa ujasiri,  na kufanya maamuzi ya wakati ujao yanayo tusubiri.

Baba Mtakatifu anatama vijana kwa sura za watu wawili akisema; Kutazama Pango  tunakutana na sura ya Yosefu na Bikira Maria, hizi ni nyuso za vijana zilizojaa matumaini na mategemeo, lakini zilizojaa maswali . Ni nyuso za vijana wanaotazama mbele na  zoezi walilo nalo ambalo siyo rahisi la kumsaidia Mungu mtoto akue. Baba Mtakatifu Francisko aliendela akitazama sura ya Maria na Yosefu na kutazama vijana wa leona kusema :  “huweza kuongelia juu ya wakati ujao bila nyuso za hawa vijana  na kushika hatamu ya uwajibikaji wa vijana wetu tulio nao”. Na kuendelaea ; Zaidi ya uwajibikaji, neno la halisi  ni deni, yaani deni tulio nalo juu ya  vijana .Kuongelea juu ya mwaka unao isha ,maana yake  ni kujisikia kuwa na wito wa kufikiria namna gani tunajihusisha na vijana kuhusu nafasi waliyo nayo katika jamii yetu.

Akielezea zaidi juu ya hilo alisema ” tumeunda utamaduni ambao kwa upande mwingine ni kuwatukuza vijana na kuwafanya wawe ni wa milele,  wakati huo huo , tumewatenga  vijana wetu, wasiwe nafasi ya hakika   ya  kuingia , kwasababu taratibu taratibu tumewatoa katika maisha ya jamii, na kuwalazimisha wahame , wawe wa kuomba omba ajira  wakati ajira hizo  hazipo  au haziwawezeshi kukidhi haja ya maisha endelevu”. ”Ni hao  tunawategemea wawe ndiyo chachu yetu endelevu, lakini  tunawabagua au kuwahukumu na  ili wabishe hodi  ambapo pia hatuwafungulii”.

Msisitizo wa Baba Mtakatifu ”Tumealikwa tusiwe kama wale wenye nyumba huko Bethlehemu , ambao mbele ya wale vijana wawili waliwambia hakuna nafasi . Hapakuwepo na nafasi ya maisha na wala ya wakati ujao. Tunaitwa kila mmoja watu kuwajibika , kwa kile kidogo , ili kuwasaidia vijana wetu  wabaki katika ardhi yao, katika nchi yao,na katika akili zao, katika uwezo wao , ambacho ni kipeo cha uhakika wa ujenzi wa maisha yao ya baadaye.Tusiwakoseshe nguvu ya mikono yao ,ya akili yao, uwezo wao wa kutabiri ndoto za mababu zao”. Iwapo tunataka  kuwasaidia maisha ya baadaye yanayostahili  , tuwatafutie ile kazi ambayo inatunza utu na huru ambayo inashirikisha  na kuleta mshikamano.Kutazama pango tunapata changamoto la kuwasaidia vijana wetu , ili wasikate tamaa sababu ya kutokukomaa kwetu , tuwatie moyo hatimaye  wawe na uwezo wa kuota ndoto na kuzipambania ndoto hizo, na waweze kukua na kujenga familia ya baba na mama wa watu wao.

Baba Mtaktifu Francisko alihitimisha kwa kusema,  mbele ya mwaka unaoyoyoma , ni vema kutafakari MUNGU MTOTO:  ni mwaliko wa kurudi katika chemchemi na mizizi ya imani yetu.Kurudi kwakwe Yesu ambaye ni imani na matumaini , na chachu na baraka. Yeye anatuinua vichwa vyetu ili kuanza upya maisha.

Sr Angela Rwezaula.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.