Mwaka 2016 umekuwa ni matukio makubwa katika maisha na utume wa Papa Francisko.
Baba Mtakatifu Francisko kwenda sehemu zilizofanyika mauaji ya kimbari huko Uholanzi
(Auschwitz) na ya huko Lisbon (Hispania), kutangazwa kwa Wosia wa Kitume ya Furaha
ya Upendo ndani ya familia na bado Papa alikutana na Patriaki Kirill na kutembelea
Lund kwa tukio la kusheherekea miaka 500 ya Mageuzi ya Kiluteri Duniani na maadhimisho
ya Mwaka Mtakatifu wa Jubilei ya huruma ya Mungu , hayo ni baadhi tu ya mambo yaliyojiri
kwa Baba Mtakatifu Francisko kwa mwaka wa 2016
Ili kupata maelezo kamili juu ya matukio haya ya Baba Mtakatifu na ni jinsi gani
alivyoyaishi kwa kipindi cha mwaka huu, Alessandro Gisotti Mwandishi wa Radio Vatican,
alimuhoji Padre Antonio Spadaro Mkurugenzi wa Gazeti la "Civiltà Cattolica", kwa mtazamo
wake wa matukio hayo ya Baba Mtakatifu, naye alipta ya kueleza kwamba "Anaamini kupembua
vipindi viwili kwa upande wa Baba Mtakatifu kwamba kwake yeye ilikuwa ni kupambanua
na huruma. Na kwamba “kwa upande wa huruma inahitaji mabadiliko,ikiwa hayo ni mabadiliko
ya ndani. Mabadilko ya Kanisa , mabadiliko ya kitume , na utume wa Papa ambaye ametafuta
namnakutekeleza ndani ya Kanisa tangu mwanzo wa utume wake.Hata hivyo aliendelea
;utume wake aliuelezea sana hata katika Wosia wa Kitume wa Papa wa Furaha ya Injili
(Evangelium gaudium).
Halikadhalika Huruma ni kutambua maana yake, ya kwamba hakuna lolote linaloweza kututenganisha na upendo wa Bwana ambaye amekuwa karibu nasi daima na ambaye daima anatusubiri. Hivyo basi ni kuonesha uso wa Mungu kwa kizazi cha leo ambacho kwao wanaonekana kuwa mbali kidogo, kama vile kioo cha gari kilichofunikwa na mavumbi. Huruma maana yake ni milango ya Mungu na Kanisa daima imefunguliwa .
Mwandishi wa habari aliuliza swali : mbele ya matukio ya mauaji ya kimbari na mateso ya huko Lesbos, Sweden, Poland, Auschwitz, na kwa maeneo ya tetemeko la ardhi Italia, Baba Mtakatifu Francisko alichagua ukimya , nini maana ya ujumbe wake ? Padre Spadaro alijibu : “Baba Mtakatifu hapendi kuelezea uchungu, kama jinsi nilivyotambua mimi ya kwamba hapendi kutoa hukumu kwa Mungu bali ni kuonesha ya kwamba Mungu yupo daima na binadamu anayeteseka; kukaa kimya maana yake ni kuwa karibu na mtu huyo na tuseme ni aina ya dawa. Jambo alilofanya papa , analifanya hata kwa watu wengi, mfano tuliona hata alipokuwa kwenye kuta za Bethlehemu, na Poland (Auschwitz), kwahiyo ni kusema anabembeleza mateso ya madonda na hiyo ndiyo maana ya kuponya,Hata hivyo ndiyo maana ya Msalaba wa Kristo, yaani kujitwisha uchungu na mateso anayoishi binadamu. Hiyo siyo kimya kitupu bali kimejaa ukaribu wa dhati.
Swali jingine lilikuwa “Juu ya Wosia wa Kitume wa Papa Francisko juu Furaha ya Upendo ndani ya familia uliyotangazwa mwaka huu, ambayo ilijitokeza hata lawama, na mabishano kwa upande wa wakatoliki . Ni namna gani Baba Mtakatifu aweze kukabiliana na lawama hizi? Padre Spadaro alisema mara kwa mara Baba Mtakatifu amesema misukosuko ni sehemu ya maisha , na hivyo ni muhimu hata kwa mchakato wa Kanisa. Tuseme baba Mtakatifu naweza kuwa na wasiwasi iwapo hakuna jambo linalotendeka au pasipokuwa na upinzani. Kwahiyo kama mchakato huo ni dhahiri basi unaunda matokeo ya ari halisi.Hata hivyo Wosia wa Baba Mtakatifu wa Furaha ya Upendo ndani ya familia ni muhimu kwasababu inajikita katika historia siyo tu kwa watu wa Mungu bali kwa kila mwamini kwenye mahusiano binafsi na Mungu. Kwahiyo wosia huo unamfanya binadamu ajitafakari na kwamba anavyojisikia na hisia zake ya kuwa familia ni kiini cha msingi wa jamii ya sasa.
Aidha Wosia huo wa kitume unazo sehemu mbalimbali Lakini sehemu ya familia ni kama kiini, licha ya uwepo wa nyufa, na migogoro, lakini inatafakarisha ya kwamba Mungu yupo katikati ya historia ya imani yake. Kwa namna hiyo ujumbe wa Wosia huo unawaalika hata makuhani, wote kuwa karibu na kila historia ya mtu binafsi.
Na mwisho lilikuwa swali: Ni jambo gani unafikiri limekuwa nyeti kwake kwake Baba Mtakatifu kwa kipindi cha mwaka huu na pia wakati wa kusheherekea miaka 80 ya Kuzaliwa hivi karibuni , kitu ambacho labda yeye hakugundua. Padre Spadaro anajibu ya kwamba ni vigumu kutambua kwani zipo sehemu nyingi katika utume wake, pamoja na kwamba haikukosekana misukosuko kwa kipindi chote .Labda jambo ambalo nimelitambua mwaka huu ni ule utulivu wake alio nao .Baba Mtakatifu daima ni mtulivu, na anatambua mapema tukio lolote linaljitokeza karibu yake , hata yale ambayo ambayo yasingempendeza.
Yeye mwanyewe alisema anakula vizuri, analala vizuri ; Padre Spadaro akaongeza "na ninaweza kuongeza anasali sana. Na kwa njia ya msingi wa sala ndani ya Mungu unamfaya awe na utulivu wa hali ya juu, jambo ambalo kusema kweli lanishangaza"
Sr Angela Rwezaula
Idhaa Ya Kiswahili Ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |