Patriaki Bartolomeo I wa Kanisa la Kiorthodox la Costantinopili, ameamua kuutangaza mwaka 2017 kuwa ni mwaka wa "Utakatifu wa Mtoto"; Aliyathibitisha hayo mwenyewe wakati wa mahubiri yake ya sikukuu ya Noeli kwa Mwaka 2016. Wito wa Patriaki wa Kiotodosi umemsukuma kutafakari maajabu ya kuzaliwa kwa Yesu kwa kutumia “ Ni neno la Mungu akafanyika mwili na akaja kwetu” na kusema ni yeye aliyekuja kwetu kama mtoto Yesu, ni Mkuu wa Ulimwengu uliokuwa unataka kumuondoa. Katika Injili ya Mathayo inasema,mnapaswa kuwatunza watoto na kuwalinda , maana ni waathirika , ni lazima kuheshimu utakatifu wa watoto hao, alisema.
Patriaki Bartolomeo anasema watoto siyo kwamba ni waathirika tu wa vita na uhamiaji wa kushurutisha, bali ni waathirika hata katika nchi zenye maendeleo kiuchumi na kisiasa ulimwenguni, na kufafanua ya kuwa ni kwa upande wa kipeo cha ndoa ,talaka za ndoa ndani ya familia, ambazo uwapelekea watoto kuathirika na aina mbalimbali za mateso ya kimwili na kiroho. Patriaki Bartolomeo vilevile alionyesha pia njia nyingine zinazoathiri watoto wa leo hii akisema ni njia ya mitandoa ya kijamii kama vile televisheni na intaneti, huo ni uchumi wa ufujaji unao wageuza watoto wakiwa bado wadogo kunaswa tayari kwenye matendo ya ufujaji na anasa.
Aidha katika ujumbe wake Patriaki alitumia maneno ya Yesu anavyoelezea watoto akisema , Kanisa letu Taktifu linatuaalika “ tuwe kama watoto, kwani kama hatugeuki kuwa watoto wadogo , hatutaweza kuingia katika ufalme wa mbingu,vilevile hasiye pokea ufalme wa mbingu kama watoto wadogo hataingia katika ufalme huo. Katika fumbo la Kuzaliwa kwa Bwana kwa upande wa Patriaki amefupisha kwa maneno ya kiitikio cha sikukuu ya kuzaliwa kwa Bwana kinachosema “mtoto amezaliwa kwaajili yetu, ni Mungu wa nyakati zote” na kusema “Mungu anajionesha katika ulimwengu akiwa na moyo safi na mwepesi kama mtoto mdogo” na kuongeza ni kwa sababu watoto wanatambua mapema ukweli, unaofichika kwa watu wenye hekima. Alimalizia kwa maneno kutoka kwa mtunzi wa mashairi ya kigiriki maneno yasemayo “Ni kwa njia ya watoto tu unaweza kuujenga mji wa Yerusalemu”.
Sr Angela Rwezaula.
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.
All the contents on this site are copyrighted ©. |