2016-12-27 15:48:00

Vijana shuhudieni kwa vitendo kwamba, ubaya hauna nafasi tena!


Baba Mtakatifu Francisko anawataka vijana wa kutoka Barani Ulaya kuonesha kwa maneno na matendo kwamba ubaya hauna nafasi tena katika historia ya maisha ya watu!" Hii ni sehemu ya wito wake katika ujumbe kwa vijana watakao kusanyika kwa pamoja kuanzia Jumatano 28 Desemba hadi  Jumapili 1 Januari 2017 huko Riga nchini  Latvia, katika Mkutano  wa 39  wa vijana wa Ulaya wa Jumuiya ya Kiekumene  Taize. Mamia elfu ya vijana wa kiotodosi, waprotestanti na wakatoliki, kutoka Ulaya wanatarajiwa kufika mwaka huu katika mji wa Latvia wakati wa  kufunga na kufungua mwaka wakiwa katika sala na takafari, wakiongozwa na kaulimbiu  “ Kwa pamoja tufungue njia ya matumaini”. Papa anasema , “ kwa nyakati zetu , watu wengi wamekata tamaa kutokana na  vurugu, ghasia, ukosefu wa haki, mateso na migawanyiko.

Watu hao wanadhani kwamba ubaya una nguvu zaidi ya yote”, lakini Papa anarudia kuwaandikia vijana;kama alivyo andika kwenye hati yake ya kumaliza mwaka wa Jubileo  ya huruma  “Misercordia et misera” ya kwamba , ni kipindi cha huruma kwa  wote na kwa kila  mmoja ,hakuna   mtu yeyote anayesahuliwa na  Mungu katika pokea nguvu yake na wema wake (21), kwa namna ya pekeee   “ ninyi vijana ambao mmechagua kuacha mambo yenu na kufanya hija ya matumaini.

Na kuongeza Papa, vijana Wakristo kutoka katika Makanisa mbali mbali kwa  siku hizo mtakazo ishi kidugu na kuonesha utashi wa kuwa viongozi wa historia, msikubali kuacha wangine wawachagulie ,maisha yenu ya baadaye,” Aidha anasema Baba Mtakatifu ; katika siku hizo ziwasaidie msiwe na hofu juu ya  udhaifu wenu, bali mkue kwa matumaini katika Yesu , Kwani ni Yesu mwenyewe anayewaamini na kuwategemea. Anamalizia akiwaomba ushuhuda wa kuiga nyayo akisema ,  kama alivyokuwa mwepesi ndugu  frère Roger na alitambua kushuhudia, nanyi pia mpate kujenga madaraja ya kindugu na kuufanya upendo uonekane kama jinsi  Mungu anavyotupenda.

Pamoja na ujumbe huo wa Papa mapema ,  Viongozi wa Makanisa na Madhehebu mbali mbali ya Kikristo  walisahini barua ya mwaliko. Kwa mara ya kwanza mkutano  wa Ulaya kwa vijana kufanyika  katika mji wenye waaamini wa Kiotodosi.  Ni hija ya matumani katika ardhi iliyoanzishwa na Frere Roger mwishoni mwa mwaka 1970. PatriakiBartolomeo; Patriaki wa kiotodosi wa  Moscow; Askofu Mkuu wa  Cantebury; Katibu Mkuu wa Baraza la Makanisa Ulimwenguni; Katibu Mkuu wa Shirikisho la Makanisa ya Kiluteri Duniani; Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa; Mwenyekiti wa Baraza la Ulaya; Rais wa nchi ya Latvia, wote hawa wameandika ujumbe kwa ajili ya kuwatia shime vijana wa Taize wanaokutana huko Riga kwa ajili ya kusali, kutafakari na kufurahia maisha ya ujana katika hali ya upendo na mshikamano wa dhati!

Sr Angela Rwezaula.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.