2016-12-26 16:00:00

Papa Francisko: chagueni mwanga kwa kukataa matendo ya giza


Kanisa linasherehekea Sikukuu ya Mtakatifu Setefano Shahidi wa kwanza kumfia Kristo na Kanisa lake kila mwaka ifikapo tarehe 26 Desemba. Baba Mt Francisko katika sala ya Malaika Bwana alitoa mahubiri kwa mahujaji wote waliofika viwanja vya Mtakatifu Petro mjini Vatican akisema: furaha ya kuzaliwa kwa Bwana inatujaza mioyo yetu hata leo, wakati liturujia ya siku inaadhimisha Sikukuu ya Mtakatifu Stefano, shahidi wa kwanza  mkristo, na kutualika, tuige mfano aliotuachia wa  kujitoa sadaka.

Ni ushuhuda mtakatifu hasa wa kishahidi kwa  Kristo, aliyeteseka kwa upendo wa Yesu Kristo, na  ni kifodini kinachoendelea kuwepo katika historia ya Kanisa kuanzia kwa Stefano hadi  nyakati sasa. Ushuhuda huo umetokana katika maelezo ya Injili ya ( Mt 10,17-22). Yesu anapowatangazia mitume wake yale atakayokumbana   wakati wa utume wake  yaani, kukukataliwa na watu na hatimaye kuhukumiwa kifo na aliwapa  tahadhari yakuwa "nanyi mtachukiwa na kila mmoja kwa jina langu" (Mt 10,22). Papa aliendelea kusema; ulimwengu unawachukia wakristo  kwa  sababu zilezile  walizo mchukia Kristo kwani Yeye alileta mwanga wa Mungu na ulimwegu ukapendelea giza  ili kuendelea kuficha mambo yao mabaya. Kwa namna hiyo kuna malumbano kati ya mafundisho ya Injili na fikra za kiulimwengu. Kumfuata Yesu maana yake ni kufuata mwanga, uliyo angaza usiku huko Bethlehemu  na kufukuza  kwa  mbali giza la ulimwengu.

Mtakatifu  Stefano akiwa amejazwa na Roho Mtakatifu , alishambuliwa wa kupigwa mawe hadi kufa kwa sababu ya imani yake kwa Kristo Mwana wa Mungu  na Mzao wa kwanza aliyekuja duniani , ambaye  anamkaribisha kila mmoja  kuchagua mwanga na maisha. Na ndiyo sababu moja msingi iliyo mfanya Yeye aje kwetu. Kwa maana hiyo Mtakatifu Stefano akiwa  anampenda Yesu na  kusikiliza sauti yake, alichagua Kristo, ambaye ni maisha na mwanga kwa kila binadamu. Kitendo cha kuchagua ukweli, yeye aligeuzwa wakati huo huo kuwa ni sadaka yenye  Fumbo la ubaya linaliendelea hata leo hii katika ulimwengu mamboleo.

Baba Mtakatifu alibainisha ubaya huo akisema ; Hata leo  hii kutoa ushuhuda wa mwanga na ukweli,Kanisa linafanya uzoefu katika sehemu tofauti ulimwenguni, ya kuchukiwa, misukosuko  hadi kufikia majaribu ya kifodini. Alisema ni ndugu wangapi  na kaka wanaendelea kubaguliwa  na kuteswa   kwaajili ya Kristo. Na kuongeza “Leo hii tuwafikirie ikiwa ni njia ya kuwa pamoja nao karibu kwa upendo kwa njia ya sala zetu na machozi yetu vilevile hatuna budi kutoa nafasi ndani ya mioyo yetu kwaajili ya Mwana wa Mungu anayejitoa sadaka katika sikukuu ya Noel, tuifanye upya furaha na utashi wa kutafuta Yeye awe  kiongozi pekee katika maisha yetu , kwa kusali na kuishi kwa fikra za kiinjili, tukitupilia mbali fikra za utawala wa ulimwengu huu. Kwa maombezi ya Bikira Maria Mama wa Mungu na wa mashahidi , tuinue sala zetu , ili aweze kutuongoza na kutusaidia daima katika safari yetu ya kumfuasa Yesu Kristo tunaye muabudi katika pango na ambaye ni shuhuda mwaminifu wa Mungu Baba.

Mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana,  Baba Mtakatifu aliwasalimia mahujaji wote akisema “ katika furaha hii ya kuzaliwa kwa Bwana ninawasalimieni nyote mliofika kutoka Italia na sehemu mbalimbali za ulimwengu, na kuwatakia tena amani na utulivu, viwatangulie katika familia zenu kwenye siku hizi za furaha na za kindugu, na kwa namna ya pekee heri ya wote mnaoitwa kwa jina la Stefano na Stefania!” Aidha alisema, “ katika  siku hizi nimepokea  ujumbe wa heri nyingi za sikukuu kutoka ulimwenguni kote na kutokana na ukosefu wa muda wa kuwajibu wote, ninawashukuru wote  na hasa zawadi ya sala zenu mnazoniombea. Alimalizia “ kwa moyo wote  Mungu awaongeze kila jema kwa wema wenu.”

Sr Angela Rwezaula.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.