Baada ya mashambulizi ya kigaidi ya Kanisa Kuu Katoliki la kikopta nchini Misri, Mons. Kyrillos Willian, Askofu Katoliki wa Kikopta wa Asiud amendika katika Gazeti la Shirika la Kipapa kwa ajili ya Msaada kwa Kanisa hitaji, juu ya hali halisi inayoendelea katika Jumuiya za Kikristo huko Misri, akisema mashambulizi ya hivi karibuni ya kigaidi yamewalete maafa makubwa na uchungu sana wakristo. Na akasema, Jumanne 20 Desemba 2016 idaidi ya watu waliokufa imeongezeka na kufikia 26 kutokana na kifo kingine cha mtoto wa miaka 10 aliyekuwa amejeruhiwa kwenye shambulio hilo; hata hivyo Askofu William anatia moyo wa matumaini ya watu akisema “pamoja na hayo ipo hali ya watu kuwa na matumaini kwa Mungu .
Hiyo ni kama vile zamani makundi ya uhaini walikuwa wakishambulia waamini wasiweze kwenda kwenye maeneo yao aidha alielezea ,Askofu juu ya mshikamano kutoka kwa watu wasiokuwa wakristo ya kwamba “wanatoa misaada ya hali na mali, kuonesha ushirikiano , na pia viongozi wa Serikali walianza mapema kutafuta wakosaji, ikiwa hata Rais wa Misri A-Sis alitamka ya kwamba asingeweza kuudhuria hata mazishi iwapo wasingekuwa wamewapata wahusika na tukio hilo, na kuongeza Askofu William “ hii ina maana yake kwetu” kuona Rais uwepo wake kwenye mazishi na kuwapa kila mmoja mkono wafiwa ,na viongozi wawakilishi wa Kanisa.
Hata hivyo pamoja na yote hayo, wasiwasi na hofu bado ipo na hasa kwa siku kukuu
za kuzaliwa kwa Bwana kwasababu Isis imetangaza.
Kwaajili ya ulinzi wa Jumuiya za Kikristo, Monsinyo William alieleza ,” Viongozi wahusika
, wametuomba ushirikiano, pamoja na kwamba ni shughuli yao kwa kuwalinda raia wao
lakini , wanataka pia kuwafundisha watu wetu namna ya kukaa chonjo, na pia kwa vijana
wetu maskout ambao mara nyingi ufanya ulinzi wakati wa Ibada za misa,watapatiwa mafundisho
yanayo husu ulinzi wa raia. Mitambo ya ulinzi imeshawekwa tayari mbele ya Kanisa kuu
, na sehemu za kulala wageni.
Sr Angela Rwezaula.
All the contents on this site are copyrighted ©. |