2016-12-22 14:30:00

kuiga mfano wa wakristo wa kwanza, na shule yetu iwe sehemu ya umoja na mshikamano”


Utoro  shuleni  , umasikini na njaa , ni baadhi ya changamoto zilizoguzisiwa siku chache zilizopita na wawakilishi wa Majimbo  wanaofundisha Dini katoliki huko nchini  Rwanda , Mkutano huomulifanyika katika Braza la Maaskofu wa Rwanda Kigali
Wawakilishi hao wa majimbo waliongea juu ya maendeleo na mapungufu yaliyotokea kwa mwaka 2016 na pia kuratibu mipango mipya ya mwaka 2017.
Pamoja na maongezi yao waligusia juu ya kazi kubwa iliyopo katika majimbo na hasa ujenzi wa madarasa mapaya na kukarabati yale yaliyopo.

Licha ya mipango hiyo lakini  bado yapo matatizo kiutawala kwa  Serikali, kutokana na uchelewashaji wa mgawanyo wa fedha mashuleni, kwasababu waliongeza, bado unakosekana umoja na  ushirikiano kati ya Serikali na Kanisa katika kuboresha mashule.Ni pamoja na ukosefu wa walimu wapya, hivyo walimu wa dini walitoa pendekezo kwa maaskofu wajadili na kupeleka  matatizo hayo katika ofisi ya Waziri wa Elimu.

Mtazamo wa  mipango ya mwaka 2017, walimu hao waliamua mambo kadhaa ambayo yanaweza kuleta ufanisi katika ufundishaji wa dini mashuleni ya kwamba , washirikiane na wazazi ili kupambana na tatizo la utoro shuleni,  waongeza idadi ya mapadre kwenye shuleni, waongeze masomo ya kiroho,ma hasa kuwaweka viongozi wa kuwasikiliza watoto na kuwasindikiza,  Kuandaa kozi za mafundisho kwajili ya kuwendeleza walimu, aidha kuboresha mafundisho ya dini katoliki  mashuleni,na mwisho kuhakikisha kwamba kila shule jimboni kuna walimu wa kufundisha dini na historia yake.


Katika kumalizia  mkutano walitoa uamuzi wa kuchagua siku ya kuhamasisha mafundo ya dini Katoliki nchi na kuchagua wiki ya mafundisho ya dini katoliki itakayowaongoza kwa mwaka 2017 yenye kaulimbiu " kuiga mfano wa wakristo wa kwanza, na shule yetu iwe sehemu ya umoja na mshikamano”
Wiki hiyo ilichaguliwa siku ya tarehe  2 Juni,2017 kufanyika Kitaifa katika jimbo ka Kibungo vilevile kufanyika kila parokia siku hiyo na tarehe  9 Juni 2017 ifanyike  kijimbo.

Sr Angela 

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.