Kardinali Angelo Bagnasco Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Italia aliadhimisha Ibada ya misa kabla ya sikukuu ya kuzaliwa kwa Bwana kwa wana Bunge la Serikali ya nchi Italia Jumanne 20 Desemba, 2016 kwenye Basilika ya Mt. Maria sopra Minerva Roma.
Akianza mahubiri Kardinali alisema , inarudi tena utamaduni wa Misa kabla ya Kuzaliwa
kwa Bwana, akiwasalimia viongozi kuanzia ngazi ya juu, bila kumsahau Monsinyo Lorenzo
Leuzzi Askofu msaidizi wa jimbo la Roma anayetoa huduma katika Kanisa lililoko katika
Bunge la Italia na kusema , anatafsiri utume wa Kristo, wa kuwapo pale watu wanapofanyia
kazi. Ni ukaribu ambao hasa Injili ina onesha njia ya kweli na makusudi ya siasa.
Tunatambua ya kwamba imani si mawazo wala sheria, bali ni kitendo cha mtu binafsi kukutana na Kristo: Alieleza, maana yeye ni mwana wa Mungu milele, mkombozi wa dunia , ni kitovu cha historia ni mwanzo wa uumbaji , na mwisho wake. Yeye ni mkate wa uzima usio isha , ni jua la matumaini, ni siku isiyo na machweo, ni joto linalopasha mioyo. Na kwahiyo bila yeye maswali makubwa hayawezi kujibiwa, na binadamu ubaki na fumbo lake mwenyewe, bila yeye tegemeo la roho na ya furaha ya maisha ,hakika maisha uangukia katika utupu.
Kardinali Bangnasco akitazama hali ya sasa ya mashambulizi ya ovyo kila kona , aliendelea
kusema uzoefu wa sasa tena unaonyesha matukio ya damu ambayo yameikumba nchi ya
Ujerman na Uturuki, na kuongezea chuki na hasira kwa watu, hivyo tukiwa katika kusali
kwaajili ya waliopoteza maisha yao na kujeruhiwa dhidi ya machafuko hayo , tumuombe
Mfalme wa amani alete juhudi za haki na maridhiano.
Uzoefu wetu tulio nao unatuakikishia ya kwamba hata furaha na mafanikio binafsi haviwezi
kamwe kuujaza moyo, Aliuliza swali ,Je ni kitu gani kinakosekana katika usalama wa
binadamu ili kuwa na hali nzuri , afya, umri , nafasi na upendo?
Kwanini tunaishi kwa kujisikia upungufu wa vitu hivyo rohoni mwetu na kujisikia
msukumo wa kwenda mbele zaidi?
Aliendelea ya kwamba jibu hili liko katika uzoefu :vipindi vizuri daima havikamiliki bali viko katika mwendo, kwa maneno zaidi ni dhaifu, wakati sisi daima tunataka kujisikia tumejazwa kabisa. Shahuku hiyo inajitokeza katka aina nyingi lakini daima ma mahali popote mikujisikia ukosefu ukosefu wa kitu flani.Haiwezekani kamwe kuishi kwa siku peke yako , ukiwa unafikiria mambo yako madogo binafsi, na hata kama ni makubwa hayawezi kuujaza moyo wako : Je kama hayo yote uliyofanya, baadaye yatakwisha , nini maana ya kijitoa sadaka katika maisha?.
Leo hii tunaishi kama vile watu ambao tumejisahau, na daima tumeweka viini machoni ya kushinda katika kazi, uwajibikaji muhimu. Na hii ni kuvutiwa na utamaduni unaotutaka tuishi kiusahaulifu. Nia kubwa hasa ni ile ya kutukataza tusifikiri, tusisikilize sauti ndani ya mioyo yetu, ya kujiuliza maswali ya msingi kama vile nini maana ya kuishi,maana ya kifo na mengine zaidi, je ni muhimu kuishi.
Kardinali aliendelea, usikila maswali hayo ndani ya mioyo yetu maana yake ni kuelekea katika uwanja wa ukweli , mambo yalivyo kweli na siyo jinsi wanavyotaka tuamini , na jinsi gani tunavyojidanyanya sisi; maana yake nafsi ytu inapata uhamsho katika uhuru, na mwisho wake ni kuona kitu gani chenye manufaa na cha kuangaza .
Aidha Kardinli alichambua maana yake zaidi alisema ni kelele na picha ambazo hujaribu
kuchuka nafasi na kuzuia ukimya uweze kuingia ndani mwetu, wa kufikiria ukweli, alionya
; hakika ni hatari kufanya mawazo yanayojenga manufaa binafsi.
Lakini basi je kuna maana gani ya maisha na hasa kwa mtazamo wa kijujuu wa kujaza
nafsi? Licha ya mafaniko ya kisayansi na kiteknolija binadamu kamili ni yule anayetambua
mafanikio hayatokani na mikono yake mwenyewe na wala ukamilifu daima kuwa ni wa
kazi yake mwenyewe , bali unatoka sehemu nyingine zaidi,na unakuja kutoka juu kama
zawadi.
Kutoka juu imejionesha kwa Jina la Yesu , Mungu anayeokoa ni Emmanuel, yaani Mungu
pamoja nasi.Yeye alikuja tangu kale kwasababu ya kutufungulia umilele,na kutuzawadia
umilele huo kwa hali ya unyenyekevu ili nasi tupate kuwa wakubwa,hata katika umasikini
, kutuvisha ili nasi tuwe matajiri wa watoto wa Mungu .
Yeye alitutafungulia kitabu cha maisha , njia ya binadamu wa kweli , katika furaha
kamilifu. Binadamu anashiriki katika kazi, lakini si mhusika mkuu, bali hiyo humsaidia
yeye kuishi.
Mwisho alimalizia Kardinali Bagnasco akisema, katika sherehe za kuzaliwa kwa Bwana,
tunataka kumuomba mtoto Yesu ili tuwe wenye hekima na huru, kwaajili ya roho zetu
na kwaajili maana wa nyakati zetu katika kujenga manufaa ya wote.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.
All the contents on this site are copyrighted ©. |