2016-12-20 15:22:00

Papa Francisko atuma salam za rambi rambi Russia!


Baba Mtakatifu Francisko amesikitishwa sana na mauaji ya Balozi Andrei Karlov wa Russia yaliyotokea nchini Uturuki, Jumatatu tarehe 19 Desemba 2016. Baba Mtakatifu anapenda kutoa salam zake za rambi rambi kwa wote walioguswa na msiba huu mzito. Anaiombea roho ya marehemu Balozi Karlov, huruma ya Baba wa milele pamoja na kuwahakikishia wananchi wa Russia uwepo wake wa karibu na mshikamano kwa njia ya sala katika kipindi hiki kigumu. Ujumbe wa Baba Mtakatifu umeandikwa kwa niaba yake na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican kwenda kwa Rais Vladimir Puttin wa Russia.

Wakati huo huo, Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa Mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican ametumia salam za rambi rambi Balozi wa Russia mjini Vatican Bwana Alexander Avdeev kufuatia mauaji ya Balozi wa Russia nchini Uturuki, Bwana Andrey Karlov, aliyeuwawa kwa kupigwa risasi wakati akifungua Onesho la Picha nchini Uturuki, Jumatatu tarehe 19 Desemba 2016.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.