Kardinali kusimikwa Rasmi Heshima ya jina la Mtakatifu Andrea della Valle.
Jumapilia 18 Desemba , Kardinali Dieudonné Nzapalainga Askofu Mkuu wa Bangui wa
Jamhuri ya Afrika ya Kati alisimikwa rasmi heshima ya jina la Mtakatifu Andrea della
Valle.
Ni Parokia ya Kanisa Katoliki mojawapo la mjini Roma lenye msimamizi wa Mtakatifu
huyo, ambapo ni utamaduni wa Vatican kwa kila anayepewa Ukardinali, kupewa jina la
heshima ya mtakatifu ambaye ni msimamimizi wa Kanisa mojawapo mjini Roma.
Kardinali Nzapalainga alipokelewa na Gombera wa Kanisa hilo Padre Carlos Gómez Ruiz
ambaye baada ya kuingia Kanisani aliletewa msalaba na kubusu kwa heshima ikiwa na
maana ya kulipokea jina rasmi la msimamizi wake wa Kanisa hilo.
Baada ya kuwasalimia waumini, alianza ibada ya misa Takatifu. Katika ibada hiyo alikuwepo
hata mwakilishi wa Katibu wa Umoja wa Mataifa, kiongozi mkuu ya operasheni ya Umoja
wa Mataifa katika nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati , Onanga-Anyanga Parfait, na
Mkuu wa Ulinzi wa Vatican Domenico Giani.
Sr Angela Rwezaula.
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.
All the contents on this site are copyrighted ©. |