Ubalozi wa Vatican nchini Ukraine, ulitoa taarifa kwamba Balozi wa Vatican nchini Ukraine , Askofu Mkuu Claudio Gugerotti alitembelea jamuiya za kikatoliki na ya Kanisa lenye liturujia ya kigiriki huko Donetsk na Luhansk kuanzia 16 -18 Desemba 2016, pamoja na ziara yake katika jumuiya mbalimbali za dini zikiwa katika maandalizi ya sikukuu, aliwafikishia salamu na baraka kutoka kwa Baba Mtakatifu Francisko. Balozi wa Papa aliwahi kutembelea Jumuiya za Zaporizhzhia na Donetsk mapema Aprili mwaka huu wakati wa sikukuu ya Pasaka.
Wakati wa mkutano na Jumuiya hizo, Balozi alizungumzia kuhusu shughuli za Papa Francisko anazofanya bila kuchoka kwaajili ya amani katika ulimwengu na shahuku yake ya kujisikia kuwa miongoni mwa watu duniani kwa ajili ya kuwaonesha ushirikiano na mshikamano wake. Aidha katika fursa la Ziara yake ya Luhansk, Balozi pia alitembelea mji wa Mytrofan ya Luhansk na Alchevsk, kuona makao ya Idara ya Mahusiano ya nje ya Kanisa la kiotodosi la Ukraine. Katika ziara yake Balozi alifuatana na msaidizi Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki la Kharkiv na Zaporizhzhia la Kanisa Katoliki inayoshughulikia miji miwili iliyotajwa.
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |