Vatican inataka wanachama wa Shirika la Usalama na Ushirikiano wa nchi Barani Ulaya kutambua biashara ya binadamu kama moja ya uhalifu wa kutisha na kufanya kila liwezekanalo kutokomeza mizizi yake. Ni maneno ya hotuba ya Munsinyo Janusz Urganczyk, mwakililishi wa Vatican katika Baraza la kudumu katika masuala ya usalama na ushirikiano wa Ulaya (Osce), Alhamisi 15 Desemba 2016 wakati wa mkutano wao wa 1124 wa Mwaka huko Vienna.
Alisema ,Vatican mara nyingi imesema juu ya shetani dhidi ya maovu ya biashara ya
binadamu, kazi ya kulazimishwa na aina zote za utumwa mamboleo, mara nyingi ulenga
unyonyaji na kuwawazia watoto. Hii imesemwa bila kuchoka kwaajili ya kuchukuliwa
hatua, kupitia taasisi za Kanisa Katoliki dunia ni kote ili kukomesha mara moja
hali ambayo ni “kansa ya kijamii”ambayo ni mojawapo ya changamoto kubwa za nyakati
zetu kama mapapa walivyosisistiza mara nyingi.
Idha aliendelea , Kwa maongozi ya mafundisho ya kanisa, hasa tangu Mtaguso wa Pili
wa Vatican uanze , kama ilivyoandaliwa na mapapa John Paul II, Benedict XVI na Francis,
taasisi nyingi kikatoliki , maparokia, mashirika ya hisani na makundi ya walei kutoka
sehemu mbalimbali za dunia zimekuwa na nia kila siku ya mapambano dhidi ya biashara
haramu, kwa njia ya kinga na kuwatunza waathirika. Akieleza njia hizo Monsinyo alisema
;
Katika kupinga mtandao halifu, waliamua kujenga imara mshikamano wa mtandao, wapate
kukutana mara kwa mara katika kuwasiliana, na pia kupitia katika vyombo vya habari
za kijamii, ambayo inaruhusu kubadilishana habari na mipango kwa haraka . Wao pia
wanashirikiana na Serikali, serikali za mitaa ili kuwatia moyo katika maamuzi yao
ya kisiasa.
Alitoa mfano ya kwamba : Kama watangulizi wa Papa Francis walilaani tatizo hili kubwa
sana na linaloficha siriili lichukuliwe hatua madhubuti .2014 akiongoza Azimio la
Pamoja na Viongozi wa dini dhidi ya utumwa wa kisasa wa mamboleo aliamua kuundwa
chombo kinachojulikana "kikundi cha Mt. Marta Group", Jina hilo baada ya kuwa ndiyo
makazi yake huko Vatican.
Hii ni muungano wa wajibu kati ya vikosi vya polisi na viongozi wa Kanisa duniani
kote, ambao una lengo, pamoja na vyama vya kijamii, ili kutokomeza biashara haramu
ya binadamu na kuendeleza mikakati ya kuzuia na kuwaunganisha na jamii ya waathirika,
pamoja na kuhakikisha huduma zao za kichungaji.
Shukrani ziwandee makundi ya kazi ,ikiwa ni pamoja na ushirikiano wa karibu kati ya
Kanisa na Polisi,wengi wanao angaika na kukaa kimya lakini wanasikia.Hawa ndiyo Papa
Francis alisema,” kinachohitajika nguvu ya pamoja, ufanisi , ari na juhudi, kwa pamoja
ili kuondokana na sababau ya jambo hili lenye utata,pia ni kukutana na kusaidia watu
ambao uanguka katika mtego wa biashara “ni ambao kwa walio wengi hawawezi kujitetea,
ni kuwaibia utu wao ,uadilifu wao kimwili na kisaikolojia, na hata maisha yao.
Katika mkataba wa agenda ya 2030 ya Dunia wa hivi karibuni na (SDGs) hasa wa lengo
la 8.9 ya wanachama wa Umoja wa Mataifa ulisaini maadili yao muhimu ya kupambana na
ukiukaji huu mkubwa wa haki za msingi za binadamu, sambamba na hiyo Vatican inawataka
Mataifa yote yanaoshiriki, kutambua kwamba usafirishaji wa binadamu kama ni mojawapo
ya uhalifu wa kutisha unaondelea kuharibu wajibu wao kimaadili, na hivyo ni muhimu
kushughulikia ipasavyo na kutokomeza ki ukweli.
Umakini lazima utolewe na hasa kwa kutokomeza uhalifu huu na hasa unapowashambulia
watoto, ambao ni watumwa , na uangukia mawindoni na kunyonywa kama vibarua au askari,
na baadaye uangukia katika mtandao wa kusafirisha madawa ya kulevya au kuingizwa kwenye
picha chafu ;ni wale wanao lazimika kukimbia kutokana na migogoro, uhatarisha kutengwa
au kutelekezwa.
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |