Wachungaji wanasema ukweli lakini wanawapokea watu kwa kile wanachoweza kutoa,
hiyo ni hatua mojawapo, kinachosalia Bwana atafikiria, ni ujumbe wa Baba Mt. Katika
mahubiliri ya asubuhi 15 Desemba 2016 katika Kikanisa kidogo cha Mt. Martha Vatican.
Akichambua Injili ya siku kuhusu utume wa Mt Yohane mbatizaji alisema; wote walikuwa
wanakwenda kumuona, hata wafararisayo, na walimu wa sheria, lakini kwa mbali yaani
kuhukumu na siyo kwa kubatizwa.Katika Injili ya siku Yesu anauliza umati walikwenda
jangwani kuona nini, mwanzi unaotikiswa na upepo, mtu aliye vaa mavazi maridadi?
Siyo anaye vaa mavasi maridadi , kwamba wavaao mavazi maridadi wanaishi ki anasa katka
majumba ya mfalme,Papa aliongezea kama katika nyumba za maaskofu.Yule mliyekwenda
kumuona ni nabii,ni zaidi ni zaidi ya nabii, kati ya waliozaliwa na wanawake hakuna
aliye mkubwa zaidi kuliko Yohane,nabii wa mwisho kwasababu baada ya yeye kuna Massiha
, alieleza baba Mt. Ya kwamba alikuwa mkubwa kwasababu Yohane alikuwa mwaminifu kwa
yale aliyokuwa ameulizwa na Bwana, n mkubwa kwasababu ni mwaminifu alisistiza papa.
Ukubwa wake unaonekana pia katika mahubiri yake
Alitumia maneno makali na mabaya kuwahubiri wafarisayo walimu wa sheria, ma makuhani,hakuwaeleza
wawe na mwenendo mzuri, bali aliwambia hivyo tu “enyi kizazi cha nyoka”Hakuwa na
lugha ya kulemba kwa maana walikaribia pale kwasababu ya kuangalia na kuchunguza ,
kamwe hawakufika kwa moyo ulio wazi bali walikuwa ni kizazi cha nyoka, Papa alibainisha
ya kamaba Yonahe , Maisha yake yalikuwa hatarini, lakini yeye alikuwa mwaminifu.
Mfano mwingine alisema hata Erode alimwambia uso kwa uso “ mzinzi wewe hauruhusiwi
kuishi njia hiyoya uinzi! Kutokana na maneno ya Yonane , Papa alitoa mfano ni leo
hii hakika kwamba iwapo Paroko katika mahubiri ya Jumapili moja adhubutu kusema
miongoni mwenu kuna baadhi ya vizazi vya nyoka na kuna wazinzi, kwa hakika , askofu
wake atapokea barua za haraka zisemazo “ mtoe paroko hapa kwasababu ametututukana
.Na Yohane lakini alikuwa akiwatukana, je kwasababu gani? Papa aliendelea ni kwasababu
ya uaminifu wa wito wake na katika ukweli.
Hata hivyo Papa alibainisha ya kwamba Yohane kwa watu wengine aliwambia mfano, watoza
ushuru,watoze kwa haki wakinzia na kile kidogo. Vilevile aliwambia maaskari wasitoe
vitisho au kukemea mtu yeyote na kwashauri watoshe na mishahara yao.Hii ina maana
ya kutokujiingiza katika vitendo vya rushwa katika dunia hii, Papa alielezea Askari
akikusimamisha anapima kama umekumywa pombe na kuanza majibishano ya hapa na pale....
Yohane alibatiza wenye dhambi , pamoja na hayo alijua amefanya kidogo maana alijua
kwa ujio wa Bwana atafanya zaidi , na waliongoka. Ni mchungaji , papa alisema, aliyekuwa
akitambua hali za watu na kuwasaidia wasonge mbele na Bwana . Yohani alikwa nabii
mmoja tu ambaye alipata neema ya kuonyeshwa na Yesu.
Pamoja na kwamba Yohane alaikuwa mkubwa na nguvui ,vilevila uhakika wa wito wake lakini
pia naye alipatwa na wakati wa kiza , na kuwa na mashaka, Papa Franncisko alisema,Yonae
alipkuwa amefungwa , alianza kuwa na mashaka hata kama alikuwa amembatzia Yesu, kwasababu
alikuwa mkombzoi si kama alivyokuwa akimfikiria.Na ndipo aliwatuma wanafunzi wawili
kumuuliza kama kweli yeye ni masiha.Yesu anasahihisha maono ya Yonahe kwa jibu la
hakika, akisema mwambieni Yohane, Vipofu wanapata kuona, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa
.Hata wakubwa wanaweza kuwa na mashaka kwa sababu ni wakubwa alisema Papa; lakini
kitendo cha wakubwa kuwa na mashaka ni jambo zuri pia zuri . kwasababu mara nyingine
ufikiria wanao uhakika wa wito wao, japokuwa inapotokea mara moja Bwana kuwaonyesha
njia mpya ya kufuata, hapo mashaka hujitokeza.
Alitoa mfano Papa na kuendelea; lakini hiyo siyo hali halisi, ni uzushi, kwasababu siyo masiha niliyekuwa namtarajia.Shetani anafanya kazi hiyo na akisaidiwa na baadhi ya marafiki au siyo!Huo ndiyo ukubwa wa Yohane akiwa nabii wa mwisho kati ya kundi la waumini walioanzia na Ibrahim, ni yule anaye hubiri toba na aliye na maneno ya kulaani kiburi , lakini mwishowe alinguka katika shaka , huo ni mpango mzuri wa maisha ya kikirsto. Kwa kifupi katika mahubiri yake alisema inabidi kusema mambo ya kweli na kuwapatia watu kile kinachowezekana kuwapatia
Na hivyo tumuombe Yohane neema na ujasiri wa kitume daima kusema mambo ya ukweli ,
kwa upendo wa kitume , kuwapokea watu na kuwapatia kile kiwezekanacho, ndiyo hatua
ya kwanza, mengineyo Mungu atafanya yote, vile vile hata neema ya kuwa na mashaka,
na hasa tunapofikia mwisho wa maisha yetu, maana kishawishi kinaweza ktujia na kujiuliza
kama ni kweli yote tuliyo amini yapo hau ndiyo ndoto za kufikrika? Yaani kuwa na majaribu
dhidi ya imani yetu,na juu ya Bwana .
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |