2016-12-15 16:50:00

Papa asema, hata Yesu hakuweza kutoa jibu mbele ya matukio ya mateso


Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi tarehe 15 Desemba 2016 alikutana na Jumuiya ya Hospitali ya watoto "Bambino Gesu," iliyoko Roma inayomilikiwa na kuendeshwa na Vatican, katika ukumbi wa Mwenyeheri Paulo IV, ulioko mjini Vatican. Akianza na salam zake alisema anafurahi kukutana nao na kuwashukuru kufika kwao na ushuhuda wao , akimshukuru kwa namna ya pekee Rais wa Hosptali hiyo Daktari Mariella Enoc kwa hotuba yake aliyoitoa. Akianza kujibu maswali ya watoto , swali la mtoto Valentina ni gumu  kuhusu watoto wanaoteseka na ugonjwa , hakuna jibu bali ni bora hili swali kubaki wazi. Hata Yesu hakuweza kutoa jibu mbele ya kesi za wakati ule , wasio na hatia walikuwa wamemeteseka katika matukio tofauti.

Yesu hakufanya mahubiri yoyote mbele ya matukio , ndiyo angeweza kufanya, lakini hakufanya hivyo.Alipokuwa akiishi hakueleza kwasabab gani kunamateso.Yesu mwenyewe alituonyesha njia yenye maana hata katika uzoefu huo wa kibinadamu, haelezi ni kwa nini kuna mateso bali alituonyesha kukubali mateso kwa upendo.Siyo kwasababu gani bali tunasekwa kwa nani. Yeyey aliteseka maisha yake kwaajili yetu na kwa zawadi hiyo ya kutoa maisha ya thamani kubwa , alituokoa.anayefuata Yesu anafanya hivyo hivyo , zaidi ya kutafuta kwanini ,bali ni kuishi kila siku kwaajili ya...

Valentina aliendelea Papa,  aliuliza swali nyeti , na la kuomba omba, kwa yule amabaye anateseka , ni ombi zuri, Paa alisema , kwamaba angeweza kusema ya kwamaba tunaweza kujifunza kutoka kwa watoto , na kugundua kila siki thamamani ya kushukuru, namna ya kusema sante.Watoto Wanatufundisha, lakini watu wazima hatufanyi. Kutokusema tu asante  kwasababu tuko mbele ya mtu ni dawa ya kuzuia  kupona kwa matumaini , ambayo ni ugonjwa mbaya sana unao ambukiza.Anaeleza Papa,  kusema asante ni kuongeza matumaini kama vile asemavyo Paulo tumekombolewa (Rm 8,24) Papa alitoa mfano , Matumaini ni Petroli ya maisha ya mkristo , inayotufanya twende mbele kila siku. Na hivyo ni vizuri kuishi kama watu wa shukrani , kama watoto wa Mungu wepesi na wachangamfu, wadogo na wenye furaha.

Akijibu swali la mtoto mwingine aliyejulikana kama Dino alisema ya kwamba, aliongea juu ya uzuri wa mambo madogomadogo.Inaweza kufikiria ni hisia ya kupoteza na hasa leo katika fikra za kuonekana na kutaka matokeo ya haraka , kufanikiwa , kuonekana .Kinyume fikirieni Yesu , sehemu kubwa ya maisha yake ilikuwa iko mafichoni , alikua ndani ya familia yake bila haraka , kila siku akijifunza , akifanya kazi na kushirikishana furaha na uchungu wa watu wake.Noel inatuelza kwamaba Mungu hakijifanya mwenye  nguvu na ukuu, bali mnyonge na mdhaifu kamaa mtoto. Alipokuwa akiongea Dino namna anavyoishi udogo huo , lakini alikuwa akiomba nafasi kubwa. Ni swali kubwa , kwani tunaishi kipindi ambacho  nafasi na muda daima  vinazidi kuwa finyo . Ni kukimbia zaidi, wakati huo na kukosa muda , na siyo tu mahali pa kuegesha magari  bali hata viwanja vya kukutana  hata muda mwafaka wa kuweza kusimama  na kubadilishana mawazo.

Papa alisisistiza ya kuwa kuna umuhimu wa kutafuta muda na nafasi zaidi kwa binadamu.Kwaufahamu wake Papa aliendela kusema kuwa katika Hospitali ya Bambino Gesu katika historia, wamejibu mahitaji yaliyokuwa yakijitokeza ; wameweza kufungua vituo vingine vya huduma, na hii ni kwasababu ya kuweza kutoa nafasi za wagonjwa na familia zao  na kwaajili ya watafiti. Na historia  hii inapaswa kukumbukwa maana ndiyo ubora wa maendeleo endelevu. Hospitali ya Bambino Gesu haikuangalia ufinyo wake bali imetazama mbele na kuunda nafasi ,na mipango ya miradi hata katika sehemu za mbali za dunia.Hii inatuabia ubora wa matibabu hautegemei tu na vyombo vya kufanyia kazi ,bali nafasi za moyo.Ni muhimu kupanua nafasi ndani ya mioyo: Papa anagogeza kusema: misaada kutoka kwa Mungu haitakosekana, ukifikiria jata nafasi  hakika za kawaida.

Swali la Tatu la lilitoka kwa Luca  akisema ni chapa gani itolwe katika Hospitali ya Bambino Gesu  paomja na iwezo wa kiufundi ambao ni kweli kuwa muhimu.Kwa upaande wa kijan Luca amabaye baada ya masomo anaingia sehemu ya kazi,  unabidi kuwafunguliw vijana na siyo tu masoko bali , Papa alitoa ushauri ya kwamba anashauri viuongi viwili , ya kwanza ni kutozima ndoto; ni muhimu kutokuzima ndoto imezuilika kwani hata Mungu katika Injili ya Jumapili 18 Desemba anawasiliana kupita ndoto, na zaidi anatualikuwa kukamilisha ndoto iliyokubwa , hata kama ni ngumu.

Ndoto inatusukuma tusisimame kutenda yaliyomema na tuzisime daima shahuku ya kutamani mipango mikubwa. Papa aliendela ya kuwa “ anafurahi kusikia ya kwamba Mungu naye ana ndoto,  hata sasa kwa kila mmoja wetu. Aidha akasema, maisha bila ndoto hayastahili kwa Mungu , na wala siyo maisha ya kikirto anayekaaa bila kufanya jambo lolote na kuridhika tu na  kuishi bila  maleongo kwa siku. Na pili ni ni zawadi , maana yake ipatiwe nafasi ya kwanza au kuitoa.  Alielezea ya kwamba unaweza kufanya kazi ukifikiria kupata tu au kujaribu kufanya kwanza kwa kijitoa kwa ajili ya faida ya wote. Hivyo kazi pamoja na matatizo yake , uweza kushirikisha kwaajili ya wema wa wengine, wakati mwingine ikawa utume. Daima tupo katika njia panda , kwa upande mwingine ni kufanya kazi kwaajili ya faida binafsi, kwaajili ya mafakio,au ili ujulikane; na kwa upande mwingine, ufuata hisia za huduma, yaami ya kujitoa, na kupenda.

 Daima mambo hayo mawili uchangamana na yanakwenda  pamoja , msingi ni  kutambua  lipi la kwanza . Kila asubuhi unaweza kusema leo napaswa kwenda pale, kufanya kazi ile, kukutana watu, kukabiliana na matatizo, lakini napaswa niishi kama anavyotaka Bwana: na isiwe kama mzigo ambao badaye unakuwa mzigo kwa watu ambao wako karibu nami, na hivyo iwe ni zawadi. Papa alisema , kazi yangu ya kufanya ni ile ya wema , kumchukua Yesu, kutoa ushuhuda, na siyo kwa maneno tu bali ni katika matendo, kwani kila siku unaweza kuondoka nyumbani ukiwa na moyo uliofungwa au uliyofunguka tayari  kukutana na kutoa huduma. Ni furaha kubwa ya moyo ulifunguka kuliko moyo uliofungwa. Papa aliuliza swali je manakubaliana? Na alimalizia akiwatakia Noel  njema na waishi na miyo iliyofunguka wakitunza roho ya familia yao.

Na Sr. Angela Rwezaula.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.