2016-12-13 16:33:00

Wenye dhambi na makahaba watakwenda mbele katika ufalme wa mbinguni.


Mahubiri ya baba Mtakatifu Jumanne 13 Desemba  katika Kikanisa kidogo cha Mt. Marta Mjini Vatican akichambua   Injili ya ya siku kutoka Mathayo  alisema  , Yesu akiwahubiria makuhani na wazee wa watu , aligusia juu wa uwajibu  wao . Wajibu wao, walikuwa na mamalaka ya kisheria , kimaadili , na kidini.


Ka njia hiyo Papa alisema Anna na Kaifa mfano walimuhukumu Yesu, na walikuwa na wakuhani na viongozi waliokuwa wameamua pia  kumuua hata Razaro , na ndiyo  hao Yuda alikwenda kubadilishana mawazo ya kumuuza Yesu na hivyo Yesu akauzwa kwa namna hiyo. 
Ni hali ya kiburi na dhuluma dhidi ya watu ambao walikuwa wamefika na kuitumia sheria kwa manufaa yao Wao walikuwa wamesahau amri 10 zilizoletwa na Musa , na sheria ilifanywa na wao,ya akili, na ya utafiti, ambayo ilifuta sheria iliyokuwa imetolewa na Bwana , Papa aliendelea wana ukosefu wa kumbukumbu inayoshambulia ufunuo wa leo.


Ni athari  kwao, kama ilivyokuwa kwa Yesu kila siku watu wanyenyekevu na masikini wanaomtegemea Bwana, hasa wale walio baguliwa wanatambua toba  hata kama hawawezi kutimiza sheria , wanateseka na ukosefu wa haki.Wanaishi kuhukumiwa ,kushukiwa na wale wenye kufanikiwa na wenye kiburi.
Yuda alikuwa ni msaliti , alifanya dhambi kubwa, na ya nguvu. Lakini Injili inasema baada ya kutubu alikimbia kuwarudishia vipande vya fedha.Je wao walifanya kitu gani,? aliuliza papa, na kuendelea hawakupata kumjibu wakisema , wewe umekuwa mshirika wetu , usijali,  aidha Sisi tunao uwezo wa kusamehe kila kitu! Na badala yake walimwambia  Happana ondoka zako kama unaweza, hilo ni tatizo lako! na walimuacha peke yake: ametengwa!

Baba aliendelea kusema Masikini msalitu Yuda kutubu kwake hakukuweza kukubalikwa na wachungaji. Kwasababu  walikuwa wamesahau ni nini maana ya kuwa mchungaji.Walikuw wasomi wa dini , ambao walikuwa na uwezo , wakifanya katekessi ya watu wenye maadili yaliyotolewa na akili zao na siyo za ufunuo wa Mungu.


Watu wanyenyekevu waliotengwa na kupigwa viboko na watu hawa, hata leo baba mkatifu alibainisha  akisema katika Kanisa mambo haya yanatokea. Kuna roho ya ukikuhaniukikuhani   maana yake kuna wakuu wa dini wanaojisikia bora hoja zao na kuwa mbali na watu , hawana muda wa kusikiliza masikini , wanaoteseka wafungwa na wagonjwa.


Alimalizia akisema Uovu wa kikuhani kukuhani ni jambo baya sana ! ni toleo moja jipya la watu hawa.Lakini baba mtakatifu alibainisha ya kwamba waathrika hawa ni sawa sawa: watu masikini, na wanyenyekevu wanaosubiri ujio wa Bwana .Baba daima alitafuta mbinu za kutukaribia , na akamtuma mwanae. Tuko tunamsubiri kwa matarajio ya furaha.

Lakini Mtoto huyo bado hajaingia katika mchezo wa watu hawa:Mtoto wake alikwenda kwa wagonjwa, masikini, waliobaguliwa, watoza ushuru, wadhambi na zaidi wakutia ahibu, makahaba.
Hata leo Yesu anawaalika  kila mmoja wetu na hata kwa wale ambao wamekumbwa na hali ya kikuhani kikuhani ,: "wenye dhambi na makahaba watakwenda mbele katika ufalme wa mbinguni.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.