Katika Jumapili ya tatu ya Majilio, Baba Mtakatifu katika omelia yake wakati wa sala ya Malaika wa Bwana katika viwanja vya Mtakatifu Petro, aliwakumbusha juu ya mafundisho ya barua ya Mtakatifu Paulo kwa Wafilipi juu ya kufurahi katika Bwana, na kwamba inahusu furaha ya kweli ndani ya moyo.
“Siyo furaha ya kijujuu au ya muda tu, ya kiulimwengu , au furaha ya kuchuma , hapana
siyo hiyo bali ni furaha ya kweli na hakika ambayo tunatakiwa kuigundua radha yake,
ni radha ya furaha ya kweli, ni furaha inayogusa moyo kiundani katika maisha yetu
wakati tukisubiri ujio wa Yesu amabo ukweija wajia na kuleta ukombozi duniani, uliletwa
na masiha aliyehaidiwa kwa Bikira Maria kule Betlehemu.
Katika kitabu cha Nabii Isaya ujumbe wa ukombozi uliotangazwa ni wa kufika kwa
Bwana ambaye ubadili mambo yote na kufanya maisha ya binadamu kuwa mapya. Mungu alikuja
katika historia ili kutukomboa kutoka utumwa wa dhambi, na akaweka hema kati yetu
ili kushirikiana nasi maisha yetu, kutuponya na majeraha na kufunga madonda . Papa
alikazia kuwa “Furaha ni tunda la tukio hilo la ukombozi na upendo wa Mungu”
“Baba Mtakatifu alibainisha ya kuwa wakristo wote tunaalikwa kuonja msisimuko wa
furaha , kwani Mkristo hasiye na furaha ,maana yake kuna jambo linalomkosa, au siyo
mkristo ! maana Mkristo ana furaha ya moyo daima , furaha yenye msukumo wa ndani
ambao umsaidia kuwa mjasiri. Bwana na atukomboe kutoka utumwa wa ndani na nje, atuongoze
katika njia ya uaminifu, mapito na kukesha kwasababu atakaporudi ,atukute na furaha
yetu kamilifu”.
Noel iko karibu na inajionesha katika mapambo barabarani, hata majumbani, vilevile
hata katika kiwanja cha Mtakatifu Petro wameweka pango.
Aliezea Baba Matakatifu kuwa hizi ni ishala za nje zinazotualika kumpokea Bwana ambaye
daima anakuja kubisha hodi , katika milango yetu ya roho, kutukaribia, na kutukaribisha
tutambue mapito yake na yale ya ndugu zetu wanaotukaribia,hasa wadhaifu na wahitaji.
mwisho Baba Mtakatifu aliiomba kushirikishana na wengine furaha ya ujio ulio karibu
wa mkombozi,ha hasa kuwatia moyo na matumaini masikini, wagonjwa, wapweke, na wale
wasiyokuwa na furaha.
Vilevile Baba Mtakatifu akiwasalimia mahujaji kutoka sehemu mbalimbali za dunia na kwa namna ya pekee salama ziliwaendea watoto na vijana wa Roma waliofika na sanamu zao za mtoto Yesu zitakazowekwa kwenye pango zilizotengenezwa ndani ya nyumbana kila mtoto aliyefika hapo alisikia ujumbe wa baba mtakatifu akiwaeleza kwamba watakapokuwa katika pango zao na wazazi wao , waombe mtoto Yesu awasaidie kupenda Mungu na ndugu, na kuwakumbusha wasali kwaajili yake kama vile naye awakumbukavyo.
Umati wa Vijana, watoto na wazazi wao kutoka maparokia ya jimbo la Roma asubuhi
ya Jumapili walisali misa ndani ya Basilika ya Mtakatifu Petro, misa iliyoongozwa
na Cardianali Angelo Comastri , ambayo ni utamaduni wa Roma kubariki sanamu ndogo
hizo za mtoto Yesu.
Papa alisema wakapokuwa katika pango zao na wazazi wao, mwombeni mtoto Yesu awasaidie
kupenda Mungu na jirani, na kumbuka kumuombea Papa kama anavyo waombea yeye.
All the contents on this site are copyrighted ©. |