Jumapili 11 Desemba Kardinali Pietro Parolini Katibu wa Vatikan, alitoa daraja
la mapadre 36 wa Shirila la Legionari wa Kristo (Legionari di Cristo) Kwenye Basilika
ya Ya mtakatidu Yohane wa Laterano.
Mapadre wapya 36 ni wa kutoka katika nchi mbalimbali na hivyo Kardinali Parolini katika
Omelia yake alisema, safari yao kutoka pande zote za dunia, Argentina , Brazir, Cile,
Ufaransa, Ujermani, Uingereza, Italia, Mexico, Marekani na Venezuela inayo sababu
moja ya msingi itokayo katika kitabu cha Yeremia , Ewe Mwenyezi Mungu wewe umenidanganya
, nami kweli nimedanganyika , wewe una nguvu kuliko mimi nawe umeshinda.(20,7)
na hiyo ni sababu ya kuacha mvuto wa Yesu Kristo kama asemavyo Mtume Paulo kwa wafilipi(Fil,3,12)
mpatie Mungu nafasi ya kwanza katika maisha yako.
Ni furaha kubwa kwa wito wao huo na aliwashukuru wote walio wasaidia kufika hatua
hiyo,kuanzia familia zao, Jumuiya za parokia wanakotoka , walimu wao wa Shirika
la Legionari wa.
Pia aliwashukuru pia walioudhuria ibada hiyo, na kuifanya iwe yenye kupendeza kwa
furaha na kuendelea , wamejitoa kwa Bwana ili wawe wamisionari wa Injili kati ya
watu.Ni kwa njia ya Roho Mkatifu katika mikono ya upako itawawezesha kutoa huduma
kama mitume wa Bwana kati ya watu, na kwasababu hiyo kila muumini anaweza kukutana
na Kristo kwa njia ya kueneza Neno la Bwana linalookoa, katika maadhimisho ya ibada
na sakramenti mbalimbali ambazo ndizo ishala muhimu za uwepo wake. Ishala hizo ugeuza
maisha na kuyatakatifuza, ni kwaajili ya huduma hiyo ya kitume ambayo ndani ya mioyo
yenu iwaongoze kila siku.
Katika somo la kwanza tumesikia maneno ya Nabii Isaya yanayochangamsha nafsi ya
utume wake , kwa maneno hayo yanapata fursa kwa upande wenu sasa “Roho wa Mungu yupo
pamoja nami , na Bwana amenipaka Mafuta (Is 61,1 )
Kiongozi wa kwanza katika tukio hili ni roho wa Bwana , kwa njia ya upako wa mafuta
muweze kuwa chumbo hai pekee cha uchunganji na mpate kwa namna ya pekee kuwa mwakuhani
wa Kristo mkitenda katika jina lake. Ni Mungu anayewateua na kuwapaka mafuta, ni Mungu
anayewatuma kwenda kupeleka habari njema kwa wenye shida , kuwafariji walio pondeka
mioyo, na kuwatangazia mwaka wa neema wa Bwana , muwe ishala inayoonyesha upendo
wake mwanifu na huruma , ambayo haichoki kamwe kutafuta kila mtoto aliyepotea, amechoka
na kuta tamaa mbele ya changamoto za sasa.
Akitoa wito juu ya utume wao ,Mapadre wapya aliwa’galisha kujiweka tayari kukabiliana
na ulimwengu huu akisema maisha yao daima ya kitume hayatakuwa ni rahisi maana kuna
hali ya kuchukiwa na pia mitafaruko ya dunia hii, bali kutokana na watu kuwa na uhusiano
wa Mungu, watakutana pia na watu wenye ut una wanao mcha Mungu.Hali ya kuchukiwa hata
Yesu mwenyewe aliitambua na ndiyo maana tunasoma katika Injili ya Yohanne 17,9.15
Yesu akisali kwaajili ya mitume katika ulimwingu hu il Mungu aweze kuwalinda na mabaya
yote kwa maana wao wanaishi katika ulimwengu bali siyo wa ulimwengu huu.
Alimalizia akiwaombea Roho Mtakatifu anayekuja washukie zaidi juu yamo awaimarishe
na familia yao ya Legionari wa Kristo ili kila mmoja wao awe mwaminifu katika wito
wake wa kikuhani.
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |