2016-12-10 17:03:00

Watu 850 nchini Italia wamekufa kutokana na ajali kazini takwimu ni Januari -Oktoba


Watu 850 nchini  Italia wamekufa kutokana na ajali kazini , kwa mujibu wa shirika la Ulinzi kazini la Vega Engineering  wakitoa  takwimu hizo zinazoonyesha ajali  kuanzaia mwezi wa Januari – Oktoba 2016.
 Ajali za watu 632 waliokufa wakiwa kazini na 218 hajali za kifo  kuanzia Januari hadi Oktaba 2016. Ni asilimia 13,3% sawa na  (ongezeko la watu 97) ukilinganisha na mwaka jana 2015 ambapo takwimu zawa n ana sasa ilikuwa watu 729 waliokufa kwa ajali kazini.


Mikoa yenye idadi kubwa ya ajali kazini ni mikoa ya kaskazini mwa Italia na Kusini .Taarifa zaidi zinasema sekta ya uchumi kwenye ujenzi diyo inayoonyesha namba kubwa ua vifo watu 96 ambayoni asilimia 15,2% ya jumla ya vifo kazini, na asimlia nyingine ya shughuli za kilimo watu 84 waliokufa asilimia ya 13,3 na sekta ya usafirishaji  na makampuni  watu 77, asimilia 12,2% ya jumla ya ajali .


Zaidi hayo  watu 97 waliokufa kwa ajali kazini  mi wahamiaji ambao ni asimilia 15,3 %  na 42 wanawake.Vifo hivi vimewakumba wat wenye umri kati ya 45-54, na matukio ya vifo hivyo ililinganiswa na idadi ya wakazi inahusisha hata zaidi ya wenye umri wa miaka 65.Taarifa zinasema ni matumaini yao kwamba kutokana na takwimu hizo ziweze kuwafikia vyomo vya habari na kuwasaidia watu wengine waweze kueneza utamaduni wa usalama kazini.

 

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vaticana.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.