2016-12-08 14:59:00

Takribani ya watu 500,000 wamesongana na hawana msaada Mji wa Maidaguri


Hali ya  mji wa Borno nchini Nigeria   ni ya wasi wasi kutokana na nguvu za kijeshi, na takribani  ya watu 500,000  wamesongana na hawana msaada  katika mji mkuu wa Maiduguri. Hawana msaada wa kitu chochote cha kuweza kuwafanya waishi, wakulima hawawezi kwenda mashambani kwao, hata masoko kufungwa, kwasabababu katika sehemu hizo zinalindwa na vikosi vya Boko Haramu.

Mwaka Jana Serikali ya Nigeria ilikuwa imetamka juu ya lishe katika Eneo hili na kutambua misaada ya kibinadamu, lakini hadi sasa watu wanaendelea kufa kwa njaa.Aidha watoto walio chini ya miaka mitano, ni kama vile wamepotea,  taarifa zinaeleza, ukosefu wa chakula umesababisha utapiamlo  na kuongezeka kwa idadi ya vifo na kusababisha dharura iwe kubwa.

Taarifa hizo zilitolewa na Madaktari wasio na Mpaka mara baada ya Mwenyekiti wa Mashirika yasiyo ya kiserikali (ONG) kutembelea nchi hizo , anaomba kuwepo na ongezeko la misaada kwa haraka ya kibinadamu , ili kuhakikisha watu hao wanapata misaada ya chakula na vifaa vya afya.Katika Taarifa iliyotumwa katika vyombo vya habari Fides inaonyesha Takwimu za makambi 11 ya wakimbizi huko Maidaguri kuanzia Mei hadi Oktaba kuwa ni asilimia 50% ya watoto wa miaka mitano wamekubwa na utapiamlo mkali, na kuongeza hatari ya vifo vingi  vya watoto 5 kila siku kati ya watoto 10,000  katika kambi ya Muna Garage na watoto 8 kila siku kati ya watoto 10,000 kwenye kambi ya Custom House.

Hata hivyo habari kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa limesema;ombi la zaidi ya dola Bilioni Moja limetangazwa ili kusaidia jamii nchini Nigeria zilizoachwa bila kitu kufuatia vitendo vya Boko Haram. Akiongea hayo Naibu mratibu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kibinadamu nchini Nigeria Peter Lundberg alitaja majimbo yenye uhitaji zaidi kuwa ni Borno, Yobe na Adamawa. Alisema kinachoendelea ni janga la ulinzi linalotokana na athari za mzozo, janga ambalo amesema sasa linageuka kuwa janga la lishe na uhakika wa chakula.

Bwana Lundberg alisesema kwa sasa kuna fursa ya kushughulikia janga hilo kwa kukidhi mahitaji husika na kwa kufanya hivyo kutaepukwa gharama za ziada. Umoja wa Mataifa unasema karibu watu Milioni Nane na nusu kaskazini-mashariki mwa Nigeria wanahitaji msaada wa chakula, malazi na huduma nyingine muhimu.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.