Pamoja na Kauli mbiu ya Mkutano huo wa Ijumaa 9-10 Desemba wa Mamea 80 wa miji kutoka duniani kote , watajadili mambo mengi zaidi ambayo yatawakilishwa na mawazo ya maoni ya umma ya Kimataifa na hasa katika mtazamo wa ongezeka la idadi ya wakimbizi katika sayari yetu, kutokana na vita , njaa na majanga ya asili. Ratiba inasema washiriki wa Mkutano huo wanatazamiwa Jumamosi 10 Desemba mchana kukutana na baba mtakatifu Francisko.
Masuala ya vizuizi vya kujenga kuta za ziada na ngome, hautazuia mamilioni ya wahamiaji
wanaokimbilia kutokana na vurugu , umasikini uliokithiri ,maradhi, ukame au mafuriko,
bali ni ushirikiano wa kimataifa kwa ajili ya mafaniko ya haki za kijamii unaoweza
kuleta ufumbuzi wa dharura hizi.Aidha maelezo kuhusu mkutano huo wa mamea katika
Chuo cha Kipapa cha Kisayansi wanayo lengo la kuanzisha taadhari ya kimataifa juu
ya tishio linaloikumba Dunia na kuweza kutafuta mwafaka kwa utulivu hasa kutokana
na kuongezeka hilo la wakimbizi katika Sayari yetu, ambayo inakadiriwa kuwa ni zaidi
ya milioni 125.
Kati ya sababu kubwa ya watu tatu robo ya dunia kuwa na haja ya msaada wa kibinadamu
,na kulazimika kuondoka katika nchi zao ni vita, na inayobaki ya dharura ya kibinadamu
inayowarudisha nyuma ni kutokakana na majanga ya asili ambayo kwa miaka ya hivi karibuni
imezidi kuongezeka na kuleta migogoro ya mazingira kama vile njaa, mafuriko na dhuroba
kali kutokana na mabadiliko ya Tabia nchi na hasa kwasababu ya ku ukataji wa miti
hovyo, na matumizi mabovu ya kilimo kwa ujumla amabayo uchangia kiasi kikubwa cha
majanga ya maszingira.
Katika mada karibia 6 watakazo gusia kwenye mkutano wa Vatican wataangalia njia
mpya ya kutafuta milango ya usalama inayojulikana kimataifa na katika umoja wa nchi
za Ulaya kwa lengo la kuwafanya watu wawe wamoja na kujali heshima za kibinadamu kwa
wakimbzi wote. Na namna ya kutafuta mbinu za kuondokana na mabadiliko ya tabia nchi.
Kwa namna hiyo Mkutano wa Mamea hao 80 kutoka dunia nzima katika nyumba ya Casina
Pio IV, utakuwa wa kutathmini mapendekezo angalau sita katika suala hili: kumaliza
vita nchini Syria, na kuzuia wimbi la wakimbizi, kuhusu Brexit ya Uingereza, kufikiria
juu ya ubunifu zaidi wa kuzaa matunda ili kuleta muungano badala ya mafarakano kwa
kuzingatia kipaumbele cha wahamiaji na ukosefu wa kazi .
Kuunda njia za kibinadamu zenye usalama na za kuaminika, kuheshimu kanuni msingi
na ufuatiliaji, kutafuta ufumbuzi wa makundi ya waathirika wa biashara ya binadamu,
kurejesha hisia ya haki na fursa za haki, vijana hawana ajira na mazingira magumu,
katika makundi ya kijamii maendeleo ya kiuchumi katika nchi zenye kipato cha chini.
Haya yote ni pamoja na mwongozo wa waraka wa Baba Mtakatifu Francisko wa “Laudato
Si”.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |