Ujumbe kutoka Baraza la maaskofu wa Burundi wakitoa pongezi kwa hatua ndogondogo zilizofanywa na wanachi katika maridhiano , na kuwashukuru wote walioshiriki kukuza njia ya maridhiano katika ujumbe wa kufunga mwaka wa Jubilei ya huruma uliyotolewa na Shirika la Habari la Fides.
Katika ujumbe wa kufungua mwaka wa huruma 2015, Maaskofu wa Burundi waliwaalika na kuwa na mategemeo ya wana Burundi kutumia mwafaka wa Jubilei ya huruma katika kufanya maridhiano , na kuweza kukaa kwa pamoja ,na kuamua ukweli katika majadiliano ya wazi,ili wapate kutatua matatizo ya nchi na ya kwamba nchi ya Burundi iweze kuishi kwa Amani,na kwa ulinzi.
Lakini katika ujumbe huo Maaskofu wanabaini ya kwamba bado kuna ndugu kaka na dada waliokimbilia nchi nyigine , pamoja na kusikia wito wao, hawakukubali kurudi makwao kwasasababu bado hajisikiii kuwa na ulinzi na usalama wa nchi. Wanauliza swali katika ujumbe huo, je hakuna cha kusahihisha kwasababu ya kutokujisikia usalama na kulindwa?
Aidha Maaskofu wanatoa malalamiko juu ya watu walio baki katika mazingira nchi ya kwamba hawaaminiani ,kwasababu inaoneka wanashitakiana wao kwa wao, wakiwa na uoga wa kusema ukweli kwa sauti kubwa, na pia wanaishi bila kuaminiana katika nyumba za jirani na kumbe ni mwafaka wa kuweza kusema ukweli na kuupokea ukweli ambao uokoa na kuleta maridhiano.
Migogoro ya siasa huko Burundi imeanza tangu mwezi wa 4, 2015 , wakati Rais Pierre Nkurunziza alipoamua kugombea kwa mara ya tatu urais, kwa kukiuka sheria ya katiba na makubaliano ya amani huko Arusha nchini Tanzania.
Tukio hilo la Nkurunzinza kwa mwezi wa 7 ilisababisha hali mbaya na fujo, ghasia , mauaji , na kupotea kwabaadhi ya wapinzani wa vyama vya kisisasa , na kuundwa kwa makundi ya kigahidi wa kupinga Nkurunziza; na machafuko hayo hadi sasa yamesasabisha mauji ya watu 500 na 300,000 kukimbilia nchi zinazopakana na Burundi.
Sr A.Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |