2016-12-07 15:50:00

Kansela Angela Merkel achaguliwa kukiongoza chama chake cha CDU


Katika hotuba yake iliyochukua sura ya ilani ya uchaguzi mkuu kansela Angela Merkel alizungumzia mada zote kuanzia kuzidi hisia za kizalendo, nchini Ujerumani na kwengineko ulimwenguni, umuhimu wa kuhifadhiwa maadili ya kidemokrasia hasa baada ya kuchaguliwa Donald trump kuwa rais wa marekani,kura ya Brexit ya Uingereza  mpaka kufikia kujiuzulu waziri mkuu wa Italia Matteo Renzi.

Katika hotuba yake  kansela Merkel alitahadharisha dhidi ya "ahadi zisizokuwa na msingi "zinazotolewa na makundi ya siasa kali aidha akikosolewa mpaka katika chama chake cha CDU kutokana na sera zake za milango wazi zilizopelekea mwaka 2015 maelfu ya wakimbizi kuingia humu nchini,kansela amesema:"Katika mkutano wao mkuu wa mwaka mmoja uliopita , walishauriana , na kila mara wanasema hali ile iliyoshuhudiwa mwishoni mwa msimu wa kiangazi 2015 juu ya wahamiaji na wakimbizi, Merkel alisema suala la wahamiaji  haitawezekana kutokea tena .

Licha ya Kansela Merkel  kusema suala la wakimbizi kuingia Ujermani halitawekana kama mwaka jana  , lakini bado libaki  changamoto kubwa katika mipaka ya nchi ya Italia ambayo inapakana na Libia katika cha Cicili , kwani ni mamia na maelfu ya wakimbizi  kila siku wanazidi kuvuka bahari ya meditranea  kuingia nchi za Ulaya. Taarifa  zaidi ni kutoka kwa Mkuu wa Operesheni ya Meli Sophia za kuokoa za Ulaya  anasema ni kati ya watu 150,000 na 200,000 wanao tarajia kuacha nchi ya Libia kujongea pwani za Italia . Eneo liitwalo Pozzalo huko Kisiwa cha Cecilia, watu wanaofika hapo wanatoa habari za kutisha juu ya woga, masumbuko wanayopata wakati wa safari ya kuvuka bahari.

Hata hivyo taarifa zinasema ya kwamba tarehe 6 Desemba wamefika wakimbizi  kutoka nchi za Libia, Siria, Guinea ya Bissau, Mali , Niger, Nigeria , Sierraleone  na ha kusikitisha namba kubwa ya watoto wadogo na vijana wasiyo na wazazi au ndugu zao.

Naye Mkurugenzi wa Ofisi ya wahamiaji wa Jimbo la Noto alitoa ushuhuda kwa jinsi gani  wakimbizi walivyosongamana, na jinsi gani wamewakaribisha katika vituo vigovidogo na hasa kuwapokea watoto wadogo na vijana, katika dharura hii, hata hivyo alisema , ni shughuli ngumu inayohitaji watu wenye uwezo wa shughuli hiyo ya mapokezi ambapo wanajikuta ni changamoto kwao.

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.