Akihutumbia katika Baraza la kudumu la Ushirikiano wa kibiashara wa nchi za nje na za Kimataifa Monsinyo Ivan Jurkovic mwakilishi wa Vatican katika Baraza hilo alisema ni muhimu kutafsiri juu ya biashara ili kufikia makubaliano na malengo ya agenda ya 2030 kwa maendeleo endelevu .
Pamoja na wasiwasi uliopo juu faida za biashara huria ya dunia na juhudi zake
zilizopigwa kwa siku za karibuni , bado juhudi zinapaswa kufanywa na Jumuiya ya Kimataifa
ili kuwawezesha wanabiashara huria wa nchi zinazopiga maendeleo ili kuingia katika
muungnano wa biashara wa kidunia.
Monsinyo Ivan alisema Uchumi wa kidunia unajitahidi kutaka kuondokana na kipeo chake
ambapo kwa mwaka 2008 -2009 ulitia uzito kwa mataifa yaliyo masikini na hata katika
uchumi wa viwanda ulio na utofauti. Mbele ya matukio kama hayo changamoto kubwa ya
kisiasa waliyo nayo kwenye Jumuiya za Kimataifa , ni ule uzito wa utandawazi ambao
lazima kuunda na kujenga utajiri unaogawanywa kwa pamoja.
Ili kufanya hivyo aliendelea Monsinyo, Taasisi za kisiasa na malengo 17 ya Agenda
ya maendeleo yaliyokusundiwa tangu 2015 hawawezi kuzuia kudumisha uwiano katika
maslahi maalum , bali lazima manufaa yawe kwa wote. Lakini hiyo inahita uangalizi
wa pande zote kwa kila mwanachama wa Jumuiya ya Kimataifa na ushirikiano kutoka katika
upande wa nchi masikini.
Alimalizia akisema Monsinyo Ivan ya kwamba kama kweli wanataka kufanikiwa katika
Agenda 2030 wanapaswa kuendeleza mipango ya maendeleo iliyokubaliwa huko (Addis
Ababa Action) Agenda mwaka 2015 kwenye mkutano wa tatu wa Umoja wa Mataifa juu ya
mikopo ya fedha kwaajili ya maendeleo , na lengo kubwa ni mabadiliko na hasa mipango
iliyokusudiwa iwekwe kwenye matendo.
All the contents on this site are copyrighted ©. |