2016-12-03 14:43:00

Baba Mtakatifu Francisko kutoa ruhusa ya kuwatangaza Watakatifu wapya


Tarehe 1 Desemba Baba Mtakatifu Francisko baada ya kukutana na kuzungumza na Kardinali Angelo Amato, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la kuwatangaza waamini wenye heri na  watakatifu ametoa ruhusa ya Baraza  kuwatangaza wenye heri  na watumishi wa Mungu katika Kanisa.

Ipo miujiza kwa maombezi ya  mtumishi wa Mungu  Yohane Schiavo aliyekuwa Padre wa Shirika la Mtakatifu Yosefu, alizaliwa 8 Julai  1903 na kuaga dunia 27 Januari 1967.Wengine ni mfiadini mtumishi wa Mungu Vincenzo Queralt Lloret, aliyekuwa Padre wa Shirika la kimisionari na wenzake 20, kati yao ni mapadre 6 wa Shirika lake, mapadre wa  5 wa Jimbo , watawa 2 wa Shirika la Upendo  na walei 7 wa Chama cha Watoto wa Mama Maria wa miujiza waliyo uwawa kikatili kutokana na imani yao  wakati wa vita vya wenyewe huko Ispania kati ya  mwaka 1936 -1937.

Mfiadini  mtumishi wa Mungu Teofili  Matulionis , Askofu Mkuu wa Kaisiadorys huko Lituania, aliyezaliwa 22 Juni 1873 na kuuwawa  20 Agosti 1962; Mtumishi wa Mungu Stanley Francisco Rother, Padre wa Jimbo aliyezaliwa 27 Machi 1935 na kuuwawa 28 Julai 1981;

Mtumishi wa Mungu Guglielmo Massaja, wa Shirika la ndugu wadogo wafransikani ;  Kardinali wa Jimbo la Roma aliyezaliwa 8 Juni 1809 na kuaga dunia 6 Agosti 1889: Mtumishi wa Mungu Nunzio Russo , Padre wa Kijimbo , na mwanzilishi wa Shirika la Watoto wa Msalaba, aliyezaliwa 30 Oktoba 1841 na kufa 22 Novembe 1906;

Mtumishi wa Mungu Yosefu Bau Burguet, padre wa jimbo , Paroko wa Masarrochos  Ispania aliyezaliwa 20 Aprili 1867 na kuaga Dunia 22 Novemba 1932; Mtumishi wa Mungu Mario Ciceri Padre wa Jimbo aliyezaliwa 8 Septemba 1900 na kufa  4 Aprili 1945. Mtumishi wa Mungu Maria Giuseppa Aubert , mwanzilish wa shirika la watoto wa mama Yetu wa Huruma , aliyezaliwa 19 Juni 1835 na kufa 1 Oktoba 1926.

Mtumishi wa Mungu Dio Luce Rodriguez- Casanova y Garcia San Miguel, mwanzilishi wa Shirika la wanawake wa utume wa Moyo Mtakatifu, aliyezaliwa 2 Agosti 1973 na kuaga dunia  8 Januari 1949. Mtumishi wa Mungu Caterina Aurelia wa Damu Azizi , na mwanzilishi wa Shirika la watawa waabuduo wa Damu Azizi wa  Bwana wetu Yesu Kristo,  na mtawa wa Shirika la  Mwenye heri Bikira Maria, Hyacinthe  aliyezaliwa 11 Julai 1833 na kuaga dunia 6 Julai 1905.

Na mwisho  ni  mtumishi wa Mungu Maria Nastal, mtawa wa Shirika la watawa wadogo la Mwenye Heri Bikiria Maria mkingiwa wa dhambi ya asili, aliyezaliwa 8 Novemba 1903 na kufariki 10 Januari 1940.

 

(Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican)








All the contents on this site are copyrighted ©.