Desemba mosi ya kila mwaka ni siku ya ukimwi duniani. Madaktari na Afrika Cuamm wanafanya juhudi ya kupambana na janga la ukimwi kwa mipango mbalimbali barani Afrika. Katika nchi ya Tanzania na Msumbiji mpango wa kuzuia na kukinga ugonjwa wa ukimwi unaoendelea kwa kasi.Novemba 30 -1 Desemba 2016 mji wa Padua umefanyika kongamano kwa ajili ya kuhamasisha nguvu la kupambana na virusi hivyo Afrika mahali ambapo tatizo la ugonjwa wa ukimwi unaendelea. Na katika mji wa Beira nchini Msumbiji , walifanya maandamano makubwa wakiwa na madaktari na Afrika Cuamm. Vituo vidogo vidogo vya afya vilivyo tawanyika katika Bara la Afrika kama vile kituo cha Bugisi Tanzania walifanya maandamano hayo ya kuhamasisha mpango huo wa kupambana na ugonjwa wa ukimwi barani Afrika kukuba haja kubwa ya kuhamasisha
Mwaka 2015, watu 15,700 wameweza kupatiwa matibabu na hawa madaktari na Afrika na daima wamekuwa mstari wa mbele katika harakati za kuzuia ukimwi. Ikumbukwe 1985 katika mkutano wa kwanza wa Madaktari wa CUAMM wa Tanzania huko Tosamaganga , kikundi cha madaktari kutoka italia wa cuamm kwa mara ya kwanza waliongelea juu ya Ukimwi wakijadili utafiti wa wanasayansi uliokuwa umefanyika katika hospitali ya Bukoba nchini Tanzania .Na baada ya mika 30 bado watu hawajatambua tatito linalo wakabili au namna ya kuweza kujizuia wasiambukizwe na ugonjwa huo. Ndiyo lengo kuu la madaktari wa Afrika cuamm kuweka mikakati ya kuwasaidia ili watu wawe na haki ya kutibiwa.
Akiongea mkurugenzi wa madaktari na Afrika Cuamm wakati wa tukio hilo Padre Dante Carraro alisema nchi 7 za kusini mwa Jangwa la Sahara wanazofanya kazi wanapambana na ugonjwa huo wa ukimwi na kuweka juhudi zaidi kwenye mipango ya kuwasaidia walioathirika na virusi hivyo.Padre Dante aliongeza ; wanakazia hasa namna ya kujikinga kuondokana na kuambukizwa kutoka kwa mama na mtoto , na kuwafundisha vijana namna ya kujikinga kwa kutumia vipimo (test and Treat). Nchini Tanzania katika mkoa wa Shinyanga wilaya ya Simiyu mwezi Novemba 2016 walianzisha mpango wa miaka mitano ya kuwauguza watu 20,000 wenye maambukizo ya ukimwi kwa kutumia mbinu ya (Test and Treat).
Nchini ya Msumbiji madaktari na Afrika wanaendelea na mbinu hizo za matibabu kwa asililima 15% ya watu wa Msubiji walio na virusi hivyo vya ukimwi, na zaidi ya hayo asilimia kubwa ni kwa ya vijana walioathirika na virusi hivyo. Uganda kaskazini kwenye mkoa wa Karamoja ; Cuamm inasimamia mpango wa Serikali wa kuzuia na kukinga virusi vya ukimwi kwa mama anapokuwa ni mjamzito .Madaktari na Afrika wanaendeleza Zaidi ya mipango maalumu ya kupambana na virusi vya Ukimwi ,katika juhudi hizo kwenye mahospitali yote wanapofanyia kazi kuhakikisha wanaendeleza tiba ya wagonjwa wanapofika katika vituo hivyo .
Sr. Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |