2016-11-28 08:06:00

Mshikamano wa Papa Francisko na waathirika wa majanga asilia!


Mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana, kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, Jumapili tarehe 27 Novemba 2016, Baba Mtakatifu ameonesha uwepo wake wa karibu kwa wananchi wa Amerika ya Kati waliotikiswa na kuguswa na tetemeko la ardhi pamoja na tufani kubwa ambayo imesababisha madhara makubwa kwa watu na mali zao hasa huko Costa Rica na Nicaragua. Baba Mtakatifu anaendelea kuungana na wananchi walioko Kaskazini mwa Italia, waliokumbwa na mafuriko kutokana na mvua kubwa iliyonyeesha hivi karibuni.

Mwishoni, Baba Mtakatifu amewaambia waamini na mahujaji waliokuwa wamefurika kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro kwamba, Kipindi cha Majilio ni wakati wa matumaini yanayofumbatwa katika uaminifu kwa Mungu na wajibu wao kama waamini. Majilio ni safari ya kumwendea Yesu Kristo ili kushiriki katika ujenzi wa Ufalme wake, unaojikita katika haki na amani!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.