2016-11-18 08:36:00

Mama Rosalia Ibrahim Kasumbilo amefariki dunia!


Sektretarieti kuu ya Vatican inasikitika kutangaza kifo cha Mama Rosalia Ibrahim Kasumbilo kilichotokea kwenye Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Mwanza, Tanzania, hapo tarehe 16 Novemba 2016. Sekretarieti kuu ya Vatican inapenda kutoa salam za rambi rambi kwa Monsinyo John Baptist Itaruma, Katibu mkuu wa mwakilishi wa kudumu wa Vatican kwenye Baraza la Ulaya wakati huu wa majonzi na msiba mzito ambao umeigubika familia yake.

Viongozi wakuu wa Sekretarieti pamoja na maafisa wote wanapenda kutoa salam zao za rambi rambi kwa Monsinyo Itaruma pamoja na familia yake kwa kumhakikishia uwepo wao, urafiki na upendo katika sala kwa ajili ya kumwombea Marehemu Mama Rosalia Ibrahim Kasumbilo, ili aweze kuonja huruma ya Kristo Mfufuka na hatimaye, kumjalia maisha yenye uzima wa milele! Marehemu Rosalia Ibrahim Kasumbilo anatarajiwa kuzikwa Jimboni Bunda, mahali anakotoka Monsinyo John Baptist Itaruma.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.