2016-11-10 16:23:00

Balozi Liviu Petru Zapirtan awasilisha hati za utambulisho Vatican!


Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi tarehe 10 Novemba 2016 amepokea hati za utambulisho kutoka wa Bwana Liviu Petru Zapirtan, Balozi mpya wa Romania mjini Vatican. Balozi Zapirtan alizaliwa tarehe 11 Julai 1947, ameoa. Katika maisha yake amewahi kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu na Jaalim. Aliwahi pia kuwa ni Balozi wa Romania nchini Lussenburg na muasisi mwenza wa Taasisi ya Italo-Rumena: Mkurugenzi wa Chuo cha masuala ya Uzamivu. Ni mwanachama wa Taasisi ya Sheria Barani Ulaya yenye Makao makuu yake huko Vienna Austria na bado anaendelea kufundisha Chuo kikuu hadi kuteuliwa kwake!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.