2016-11-07 14:58:00

Monsinyo Emmanuel Dessi Youfan ateuliwa kuwa Askofu wa Bafoussam


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Monsinyo Emmanuel Dessi Youfan kutoka Jimbo Katoliki la Bafoussam, Cameroon kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo Katoliki Bafoussam. Askofu mteule alizaliwa tarehe 7 Agosti 1967 Jimboni Bafoussam. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikuhani, tarehe 16 Juni 2001 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre.

Tangu wakati huo amebahatika kuwa ni Paroko na Msimamizi wa Madhabahu ya Bikira Maria;  na baadaye akateuliwa kuwa Makamu Askofu. Na kuanzia mwaka 2010 – 2012 alipelekwa na Jimbo kwa ajili ya masomo ya juu taalimungu huko Paris, Ufaransa. Tangu mwaka 2012 amekuwa ni Paroko na Makamu wa Askofu Jimbo Katoliki la Bafoussam, nchini Cameroon.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.