2016-10-28 06:34:00

Balozi Oren David wa Israel awasilisha hati za utambulisho Vatican


Baba Mtakatifu Francisko Alhamisi, tarehe 27 Oktoba 2016 amepokea Hati za Utambulisho za Balozi wa Israel mjini Vatican, Bwana Oren David, ambaye ni mzaliwa wa Israel na mwenye elimu ya shahada katika Mahusiano ya Kimataifa, na Shahada ya pili katika Sayansi ya Siasa. Bwana Oren David amewahi kushika nafasi mbali mbali za Utumishi na Elimu ya juu kiutendaji katika taasisi na vitengo tofauti tofauti kwenye Bara la Marekani na Bara la Ulaya. Kabla ya kuteuliwa kuwa Balozi wa Israel nchini Vatican, alikuwa Balozi wa Israel katika Moldavia na Malta.

Na Padre Celestine Nyanda.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.