2016-10-24 09:59:00

Nia ya sala ya jumla ya Papa Francisko kwa mwezi Oktoba, 2016


Baba Mtakatifu Francisko katika nia yake ya jumla kwa Mwezi Oktoba, 2016anawataka waandishi wa habari kujizatiti kikamilifu katika kukuza na kudumisha mchakato wa huduma ya watu kukutana. Baba Mtakatifu anasema, mara nyingi anapenda kujiuliza Je, ni kwa kiasi gani vyombo vya mawasiliano ya jamii vinaweza kutumika katika mchakato wa ujenzi wa huduma ya watu kukutana?

Baba Mtakatifu anapenda kuona waandishi wa habari wakitoa habari ambazo zitasaidia katika mchakato wa ujenzi wa utu, heshima ya binadamu na mafao ya wengi. Baba Mtakatifu katika ujumbe huu kwenye video unaonesha wadau mbali mbali wa vyombo vya upashanaji habari ambao Baba Mtakatifu anapenda ujumbe wake uweze kuwafikia. Waandishi wa habari, daima wachangamotishwe kuheshimu ukweli na kujikita katika msingi thabiti wa maadili. Baba Mtakatifu Francisko anahitimisha nia yake ya jumla kwa mwezi Oktoba kwa kuwaalika waandishi wa habari kusaidia mchakato wa kusambaza nia hii, kwa kusema “Ndiyo” kwa kila mwandishi wa habari kutoka kwenye vituo vilivyooneshwa katika video hii.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.