2016-10-24 16:00:00

Askofu Faustin Ndjodo ateuliwa kuwa Askofu mkuu wa Garoua, Cameroon


Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi la kung’atuka kutoka madarakani lililowasilishwa na Askofu mkuu Antoine Ntalou wa Jimbo kuu la Garoua, nchini Cameroon. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu amemteua Askofu Faustin Ambassa Ndjodo kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Garoua. Kabla ya uteuzi huu, Askofu Ambassa alikuwa anahudumia Jimbo Katoliki la Batouri.

Askofu mkuu mteule  Faustin Ambassa Ndjodo alizaliwa kunako tarehe 26 Julai 1964. Mara baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisis, kunako tarehe 26 Julai 1997 akapewa Daraja ya Upadre. Tarehe 3 Desemba 2009 akateuliwa na Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Batouri, nchini Cameroon na kuwekwa wakfu kuwa Askofu hapo tarehe 31 Januari 2010. Tarehe 22 Oktoba, 2016 Baba Mtakatifu Francisko akamteua kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Garoua, nchini Cameroon.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.