2016-10-20 15:58:00

Ikulu ndogo ya Castel Gandolfo sasa ni Jumba la Makumbusho ya Vatican


Kwa mara ya kwanza katika historia ya Kanisa, Ikulu Ndogo ya Castel Gandolfo iliyoko nje kidogo ya mji wa Roma, Jumamosi, tarehe 22 Oktoba 2016 itafunguliwa rasmi na kuanza kutembelewa na mahujaji pamoja na wageni mbali mbali wanaofika mjini Roma. Kwa muda wa miaka miwili, Bustani maarufu sana za Castel Gandolfo zilikuwa zinatembelewa na wageni kutoka sehemu mbali mbali za dunia.

Hatua inayofuata kwa sasa ni kufungua vyumba vilivyokuwa vinatumiwa na Mapapa wakati wa mapumziko ya majira ya kiangazi, Ikuku Ndogo ya Castel Gandolfo. Taarifa zinasema kwamba, Ikulu Ndogo ya Castel Gandolfo ambayo kwa sasa inakuwa ni sehemu ya Makumbusho ya Vatican inaweza kutembelewa wakati wote. Kwa wale wanaotumia mitandao wanaweza kupanga siku maalum ya kutembelea kwa kutumia mtandao kwa anuani ifuatayo: www.museivaticani.va

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.