2016-10-15 13:16:00

Papa ; Kanisa linawapenda kwa dhati wazee


Katika Mazingira ya kuadhimisha Siku ya Kitaifa ya wazee, mababu na mabibi hapa Italia, Papa Francisko  mapema Jumamosi tarehe 15 Oktoba 2016 amewapokea wawakilishi na viongozi wa  Chama kinachounganisha vyama vya Wazee Italia, katika wiki hili linalojuikana kama ni  Siku ya Wazee, Mabibi na Mababu.  Baba Mtakatifu alikutana na kundi la wazee  mabibi na Mababu na wasaidizi wao, na kwa pamoja walitafakari na kutolea sala na maombi yao kwa Mwenyenzi  Mungu.  

Hotuba ya Papa kwa wazee, ilionyesha upendo wake wa dhati kwa mabibi na mababu na kwa maneno yaliyotolewa na Rais wa Vyama vinavyowauganisha wazee hapa Italia. Papa  alionyesha pia kutambua hali ngumu ya maisha inayowakabili wazee wengi ,  hasa upweke na maradhi , akisema  Kanisa liko pamoja nao katika umoja wa kiroho .

Na kwamba Kanisa , linawaheshimu sana wazee na linawapenda  na kuwashukuru kwa heshima kama sehemu muhimu  ya jamii na hasa  jamii ya Kikristo,  likitambua kuwa wao ni  mizizi na hazina ya  thamani sana,  ghala la kumbukumbu zote za utendaji wa watu katika miaka ya umri wao. Papa aliendelea kwamba, uwepo wao ni muhimu, kwa sababu, kizazi kijana kinahitaji uzoefu wa wazee katika maisha , na hivyo wanakuwa ni hazina ya thamani, hata katika kutazama mwelekeo wa siku zijazo,  matumaini na uwajibikaji. Ukomavu wao na hekima walizokusanya katika miaka yao,ni msaada kwa vijana, kukua katika  njia  nyoofu kwa ajili ya dunia bora kwa siku zijazo.

 Aliongeza  wazee, kwa kweli, hata katika majaribu magumu zaidi, wengi wao wameonyesha kutopoteza imani kwa  Mungu na katika kujenga maisha ya kiroho yaliyo bora zaidi kwa baadaye. Wao ni kama miti unaoendelea kukua na  kuzaa matunda: hata chini ya uzito wa miaka,  hutoa  mchango wao  kwa ajili kufanikisha ustawi wa  jamii, katika maadili na tamaduni thabiti wa maisha.

Na kwamba idadi kubwa ya wazee kwa ukarimu wao hutumia muda wao na vipaji walivyo jaliwa na Mungu , kutoa msaada kwa wengine licha ya unyonge wa mwili. Papa Francisko ameeleza kwa kutazama kazi zinazofanikishwa na wazee katika Kanisa ambamo wengi hufanya kazi za kujitolea kanisani kama  makatekista  au  kuwa viongozi wa Kanisa kazi nyingine kama  mashahidi upendo.  Na si katika Kanisa tu lakini  hata ndani ya familia huduma ya mababu na mabibi ina thamani si tu kuwapeleka watoto mashuleni lakini siku hadi siku wanazokaa na wajukuu zaom hurithisha uzoefu wa maisha, maadili ya kiroho na utamaduni ya jamii na watu! Katika nchi ambazo hupita katika kipindi kigumu cha mateso makali ya kidini , ni mambau namabibi wanaodumisha imani na kuipitisha kwa vizazi vipya, na hivyo ndiyo maana huwa na watoto wanaobatizwa hata katika  mazingira ya mateso na ukatili.

Papa alieleza na kutoa mwaliko kwa watu wote akisema kuwa  sote tumeitwa kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya utamaduni wa maisha, kushuhudia kwamba kila msimu wa maisha ni zawadi kutoka kwa Mungu na ni ina uzuri wake wenyewe na umuhimu wake, ingawa kuna alama za udhaifu.  Na kwamba , mbele ya uso wa watu wengi wazee ambao, kwa mujibu wa uwezo wao, wanaendelea kutumikia wengine, kuna watu wengi ambao wanaishi na maradhi ya kimwili licha ya ulemavu wakihitaji  msaada.

Baba Mtakatifu Francisko aliutumia muda huo kumshukuru Mungu kwa  watu wengi na miundo mbalimbali iliyowekwa wakfu kwa ajili ya kuhudumia wazee kila siku na kuboresha mazingira ili kwamba, kila mtu aweze kuishi kwa heshima hadi hatua hii muhimu ya maisha yao. Hivyo Taasisi na  nyumba za wazee panatakiwa kuwa ni  maeneo yenye  ubinadamu na upendo dhahiri , kwa wazee wote hata wale wenye  dhaifu na waliosahaulika au kupuuzwa,wawweze kutembea pamojana wengine kaka na dada. Papa alieelza na kukamilisha hotuba yake kwa kutoa shukurani za dhati kwa wazee,  kwa huduma, na kwa  mfano wao wa upendo, kujitolea na hekima, wakionyesha  ujasiri katika kutoa ushahidi juu ya maadili haya, na kwa tabasamu lao lisilokuwa na mwisho. 








All the contents on this site are copyrighted ©.