2016-09-30 16:17:00

Papa aanza ziara ya Kimataifa ya 16, Georgia na Azerbaijan


Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa hii 30 Septemba , majira ya saa tisa za mchana, aliwasili katika uwanja wa kimataifa wa Tbilisi nchini Georgia ambako ameianza ziara ya Kitume ya Kimataifa ya 16,  akianzia na Georgia atakapokuwa hadi  kesho Jumamosi mchana, kisha  ataondoka kuelekea Azerbaijan ambako atakuwa hadi siku ya Jumapili tarehe 2 Oktoba 2, 2016. Papa katika ziara hii, amepeleka ujumbe wa amani na maridhiano kwa raia wa mataifa hayo, na pia kwa nia ya kuimarisha umoja, mshikamano na imani kwa wafuasi wa Kristo.

Mara baada ya kuwasili Tiblisi, alipata mapokezi yenye hadhi ya heshima yake. Na  majira ya saa kumi saa za jioni kwa saa za Georgia, , alikutana na  Viongozi wa serikali, vyama vya kiraia na wanadiplomasia wanaowakilisha nchi zao katika nchi ya Georgia.

Katika hotuba yake amemshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumpatia fursa hii ya  kutembelea taifa la Georgia, kukutana na kubadilishana mawazo na watu wa  tamaduni  na staraabu mbalimbali,   ambako kwa upande wa Ukristo , kuna urithi wa mahubiri ya Mtakatifu Nino, wa karne ya nne, aliyeacha utambulisho imara wa Ukristo na tunu za maadili.  Aidha Papa alikumbuka ziara iliyofanywa na mtangulizi wake, Mtakatiifu  Yohane Paul II katika taifa hilo, ambako mbegu ya Ukristo, inaonekana kuchanua  mfululizo katika  utamaduni watu wa Georgia.

Papa Francisko ameeleza na kutoa shukurani zake za dhati kwa , Mheshimiwa Rais, kwa mwaliko wake na kwa maneno mazuri na makaribisho mazuri , kwa niaba ya Mamlaka ya Serikali na raia wote wa  Georgia.

Papa akitazama kwa kina historia ya taifa la Georgia,  tangu zama za kale hadi leo hii , ametoa wito kwa taifa hili, lizingatie  kudumisha uhuru wake kwa kujenga demokrasia imara katika taasisi zake zote , ili raia wake wote kwa pamoja , waweze tembea katika barabara ya maendeleo na umoja wa kitaifa.  Papa ametoa mwaliko huo huku akionyesha kutambua  kwamba, kufanya hivyo nilazima mtu alegeze moyo na kukubali kuwa mtumishi kwa manufaa ya wengine.   Na pia ameonyesha matumaini yake kwamba,  njia ya amani na maendeleo,  na juhudi za pamoja zitaendelezwa kwa ajili ya kufanikisha manufaa ya watu wote, na pia kwa ajili ya ujenzi wa mazingira ya utulivu, haki na kuheshimu sheria , ukuaji wa uchumi na kuongeza fursa  za maendeleo kwa wote.

Na kwa upande wa Kanisa Katoliki , amelitaka liwe mstari wa mbele kushiriki katika juhudi zote za maendeleo ya binadamu kupitia  matendo ya huruma , na kugawana  na kushiriki za katika hali zote furaha na wasiwasi wa watu Georgia. Ni muhimu kutoa mchango wa Kanisa katika shuguli zinazolenga kuleta ustawi na amani  kitaifa. Kanisa ni lazima kufanya kazi, karibu na mamlaka na vyama vya kiraia.

Papa Francisko ameeleza na kuonyesha  matumaini yake ya dhati kwamba mchango wa kanisa Katoliki ambalo limekuwa nchini huo kwa karne nyingi, kwa namna ya kipekee, litanedelea na kazi zake za kukuza ubinadamu na matendo ya huruma , likishiriki katiak furaha na wasiwasi wa watu wa Georgia , na kutoa mchango wake kw ajili ya mema na manuaa ya kitaifa, kupitia ushirikiano wa dhati na mamlaka za utawala mahalia kwa  manufaa kwa jamii ya Georgia. Na pia ameshukuru wale wote walioweza kuushuhudia utamaduni wa kikristo wenye kuwaunganisha na kazi zinazowajali watu wahitaji zaidi na katika kufanya upya na kukuza majadiliano na Kanisa la Kale la Kiotodosi la Georgia na jumuiya zingine za kidini. 








All the contents on this site are copyrighted ©.