Mwandishi wa habari idhaa ya kiswahli wa Radio Vatican Mama Janeth Mhela Alhamis 29.10.2016. ametunikiwa zawadi ya heshima , medali ya msalaba kwa lugha ya kilatini “Pro Ecclesia et Pontifice”kwa kwaajili ya shukrani katika huduma ya kutumikia Radio ya Papa.
Mama Janeth Mhella wa idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican amekuwa mwafrika wa kwanza kutunukiwa zawadi ya heshima na Papa Francis , kwaajili ya utendaji mzuri wa kazi na huduma ya Kanisa.
Ametunikiwa zawadi kwa heshima na baba mtakatifu Francis medali ya msalaba wa heshima na cheti kwa ajili ya kutambua huduma nzuri aliyoifanya.
Zawadi hizo amezipokea kutoka mikononi mwa Monsinyo Dario Edoardo Viganò, Mwenyekiti wa Sekretarieti ya mawasiliano wa Vatican kati ya watu wengine watano waliopata zawadi ya heshima ya kitakatifu katika sekretarieti ya mawasiliano.
Mwisho wa mwezi wa Octoba 2016 Janeth Mhella anastaafu kutoka katika Radio Vatican baada ya kufanya kazi kwa miaka 23.
Sr Angella Rwezaula.
All the contents on this site are copyrighted ©. |