(Vatican) Kudumisha ukweli wa imani ya Mkristo kwamba Yesu Kristo ni Bwana, aliyekufa na kufufuka, na kamwe hatakufa tena , ni kiini msingi katika imani ya Mkristo, anayotakiwa kuishuhudia daima na popote, kushuhudia ukuu, utakatifu na ushindi wake dhidi ya mauti. Kwa muhtasari , Papa Francisko, alieleza katika homilía, aliyoitoa wakati wa Ibada ya Misa, mapema Jumapili iliyopita, katika Uwanja wa Kanisa Kuu la MtakAtifu Petro Vatican. Nia Kuu ya Ibada, ilikuwa adhimisho la Jubilee Maalum ya Makatekista , katika mwaka Mtakatifu wa Huruma, kama ilivyopangwa ifanyike Jumapili ya 26 ya Kipindi cha kaiwada katika Kalenda ya Liturujia ya Kanisa Katoliki.
Baba Mtakatifu Francisko, alilitafakari fumbo la Pasaka, kiini cha imani ya Kikristo , akiitaja Ekaristi kuwa sawa na mapigo ya moyo yanayotoa uhai kwa kila jamb o, na hasa katika kutangaza fumbo la Pasaka , Mbiu Kuu ya kwanza kupigwa kwamba, Bwana Yesu aliyekufa na kufufuka, yu hai hayumo tena kaburini. Papa aliendelea kueleza juu ya fumbo hili la Pasaka ambamo Yesu anayonyesha upendo wake usiokuwa na kipimo kwa watu wote, anayetolea maisha yake msalabani kw aupendo mkuu, kwa ajili ya kumkoboa binadamu dhidi ya dhambi zake. Papa alieleza na kuwahimiza Makatekista kushuhudia ukweli huu , Yesu alikufa msalabani , kuzikwa kaburi na kufufuka . Sasa yu hai, yuko karibu nasi na anatusubiri kila siku. Papa alieleza kuwataka Maktekista kuzingatia hilo kama jambo la lazima katika ushuhuda wao na mafundisho yao.
Maelezo ya Papa yalilenga katika masomo ya siku na hasa Injili ya Jumapili ambamo mlitolewa mfano wa mtu maskini Lazaro na mtu tajiri akisema kwamba , , mfano huu unaolenga kutufundisha jinsi Bwana anavyowajali na kuwahudumia watu kupitia sisi wenyewe, na hasa wale ambao wanapuuzwa katika maisha ya hapa duniani, na jinsi itakavyokuwa baada ya kifo chetu. Hivyo mfano huu wa Lazaro na Tajiri , unatupa fundisho la kutafakari dhamiri na wajibu wetu katika kupelekea habari njema kwa watu wengine na hasa kwa wale wanaohitaji zaidi, yaani maskini wa roho.
Baba Mtakatifu aliendelea kulenga katika maadhamisho ya Jubilee ya Makatekista katika mwaka Mtakatifu wa Huruma na kuhoji iwapo walikuwa tayari kutimiza wajibu wa kupeleka habari njema ya wokovu kwa watu wote bila kujisikia wachovu. Na iwapo wanadumisha ujumbe msingi wa imani kwamba Bwana alifufuka na yu kati yetu. Aliwaonya Makatekista kwamba, katika kazi zao zote, hakuna jambo jingine lililo muhimu zaidi ya Kutangaza ushindi wa Kristo dhdi ya mauti. Na kwamba, kila jambo linalo husishwa na ukweli huu msingi huzaa matunda mazuri na hasa iwapo litazingatia kaulimbiu ya Pasaka. Na kwamba utendaji wowote unaotenganishwa na ukweli huu, kwamba Kristo alikufa na kufufuka na sasa yu hai kati yetu , hupoteza nguvu yake.
Kwa Maneno hayo, Papa alitoa baraka zake kwa Makatekista wake kwa waume , akimtaka kila mmoja wao afanywe upya kila siku kwa furaha ya kuwa mtangazaji wa mbiu ya Injili kwamba, Yesu alikufa na kufufuka, sasa yu hai na anaishi kati yetu na Yesu anampenda kila mmoja wetu. Papa aliomba uwezo wa Kristo, uwapatie wote ujasiri na nguvu za kuishi na kutangaza amri ya upendo na kuondokana na upofu na huzuni za kidunia. Aliwaombea ili wawezeshwe kuwaona maskini kama Lazaro, ambao Injili haikuwapuuza, lakini daima huona umuhimu wao na hujifunua wazi mbele ya watu wote.
All the contents on this site are copyrighted ©. |