Baba Mtakatifu Francisko katika Katekesi yake kwa majuaji na wageni, aliendelea kutafakari mwaka wa Huruma akiainisha matendo ya huruma ya Yesu, yaliyotajwa katika Injili na sauti ya Yesu, inayowaita waliokata tamaa, maskini na watoto wadogo na dhaifu wote wasio kuwa na nguvu za kujiinua wenyewe, kutegemea nguvu za kipekee za Mungu” kama ilivyoandikwa katika Injili ya Matayo 11: 28-30 ” Njoni kwangu ninyi nyote msumbukao na kulemewa na mizigo , nami nitawapumzisha”.
Baba Mtakatifu amehimiza kwamba , tunapokuwa dhaifu, tunapokuwa hatuna uwezo, tusikate tamaa bali tuwe na imani katika uaminifu na huruma ya Mungu; tumwendee Yesu kwa ajili ya kuupata msaada wake wa kipekee.
Papa alieleza na kutafakari utendaji wa mahujaji wengi katika Mwaka huu wa Jubilee ya Huruma, mahujaji toka duniani kote , ambao wanatafuta kupita kupita katika vizingiti vya Mlango Mtakatifu wa Huruma, wakitafuta msaada na wokovu wa Bwana wa maisha. SAmesema kuwa,wengi wanaiendea huruma ya Bwana isiyokuwa na kipimo. Na katika kufanya hivyo wanagundua kwamba, nira ya Yesu ni nyepesi , kwa kuwa Yesu hubeba mizigo mizigo ya dhambi za binadamu , na kwa mateso aliyopitia katika ubinadamu wake, ameionyesha njia ya wokovu, kwamba ni njia iliyojaa miba na mateso.
Baba Mtakatifu ameendelea kueleza juu ya kushiriki katika mateso ya Yesu akisema kuwa, kwa kuyashiriki mateso tunaweza tambua mapenzi ya Mungu juu yetu, na hivyo kupata uwezo wa kutambua faraja za kweli ndani yake, na katika kuushiriki mpango wake wa wokovu.
Kwa maelezo hayo, Papa aliongeza , hivyo Yesu anatualika sote, pia kujifunza kumuiga katika kuwahudumia maskini na wa wote wanaoteseka. Amemsihi kila mmoja wakati wote kutochoka au kukata tamaa na kuondoa woga katika kujenga matumaini mpya kwa Yesu, kwa kuwa Yesu kamwe hamtelekezi mtu. Hivyo sote na tumwendee Kristo , tukiwa tumejawa na imani kwake , kama mkombozi pekee, tukijipumzisha ndani yake na kufurahia kumtumikia.
Baada ya Katekesi alitoa baraka zake za kitume akionyesha matumaini yake pia kwamba, katika Sikukuu ya kutukuzwa kwa Msalaba, bila shaka kila mmoja ameweza kuamusha hisia mpya katika maisha ya kumfuata Yesu.
All the contents on this site are copyrighted ©. |