(Vatican Radio) Jumamosi asubuhi katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican, , kuliunguruma, ngoma , nyimbo, vigelegele na vifijo, kutoka kwa maelfu ya wafanyakazi wa kujitolea na wahudumu wanaofanyakazi katika taasisi za misaada, waliomiminika katika Uwanja wa Kanisa Kuu hili, kwa ajili ya kuadhimisha Jubilee yao maalum ya mwaka wa Huruma.
Pamoja na nyimbo na ngoma, pia shuhuda nyingi zilitolewa na watu wa kujitolea wa pande mbalimbali za dunia.
Papa Francisko , akishiriki sherehe hizi , katika hotuba yake , alizungumza juu ya mandhari ya upendo, akilenga katika aya za Mtume Paulo, alimoandika juu ya upendo kwamba, hata kama nikinena kwa lugha za malaika , lakini kama sina upendo mimi nimekuwa kama sauti ya debe tupu au kengele. Hata kama nina kipaji cha kutangaza ujumbe wa Neno la Mungu na kujua kila siri zote au kuwa na uwezo na imani kali hata ya kuhamisha milima , lakini kama sina upendo mimi ni kitu bure …
Baba Mtakatifu alitafakari na kusisitiza kwamba , mafundisho haya yanaonyesha kwa uthabiti wa hakika katika imani ya mtu isiyoyumba . Na kwamba kamwe upendo wa Mungu hautakiwa kunyauka katika maisha ya muumini na katika historia yake. Upendo wa Mungu daima lazima ujitokeza upya katika utendaji wote wa kazi , na nguvu zote na katika vishawishi vyote kama matunda ya imani kwa Kristo.
Baba Mtakatifu alisisitiza kwa nguvu Kwamba , Mtume Paulo , anazungumzia upendo wa kwelli na halisi na si maigizo au utendaji wa kufikirika usioleweka , lakini ni halisi yenye kuonekana na kuguswa, kwa kuwa ni utendaji wa mikono , wenye kieleleza halisi kinachoonyesha upendo mkubwa wa Yesu Mwenyewe. Yesu alionyesha na anaendelea kutuonyesha upendo wa Mungu kwa kufa msalabani.
Katika uso wa ukweli huu, Papa Francis aliongeza kusema kwamba, hatuwezi kukaa kimya au kutojali. Kanisa haliwezi kujifanya halioni au kutegea mgongo aina nyingi za mahangaiko na mateso halisi ya watu hasa watu maskini. Badala yake hujali na kupiga ukelele wa huruma kwa niaba ya maskini. Huruma yenye kuonekana katika utendaji madhubuti , kupitia misaada yake kwa watu wahitaji.
Papa aliendelea kusema kuwa , huruma hii katika ukweli wake,inapaswa kuwa kitambulisho cha kuonekana katika maisha yetu ya kila siku, ikionyesha wazi utendaji wa Mungu kati yetu. Na kwamba Mkusanyiko huu mkubwa watu wa kujitolea waliofika katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, unawakilisha wahudumu wa upendo na huruma ya Mungu toka pande zote za dunia.
Papa amewataja wahudumu hawa, kuwa ni watu muhimu na maalum kwa Kanisa , ambao kila siku , katika hali ya kimya kimya, na mara nyingi , katika kazi zao za kujitolea, huonyesha sura ya huruma ya Mungu . Papa aliwahimiza daima kuwa tayari kutoa msaada na mshikamano kwa jamii na waendelee kutenda kazi yao kwa furaha na unyenyekevu . .
Shrehe za maadhimisho hay aya Jubilee ya wahudumu wa upendo ni kama dibaji ya sherehe za Jumapili tarehe 4 Septemba 2016, ambamo Baba Mtaktifu Francisko ataongoza Ibada ya mIsa kwa nia kumtangaza Mwenye Hei Mama Twreza wa Calcutta kuwa Mtakatifu. Fadhila na upendo wa Mama Tereza wa Calcutta kwa watu maskini zinajulikana duniani kote. Hivyo utendaji wake ni kioo kinacho oneysha cha huruma ya Mungu kwa watu wote bila mipaka.
All the contents on this site are copyrighted ©. |