2016-09-02 15:09:00

Masista Watatu waliouawa Burundi wakumbukwa


Masista wa Mtakatifu Xaviery,katika kuikumbuka tarehe 7 Septemba ya 2014,ambamo Masista wenzao watatu waliuawa kikatili wakiwa nchini Burundi na watu wenye silaha kali  wasiofahamika, wamekumbukwa na   Masista wenzao  kwa kuchapisha kitabu chenye jina : "Nenda Kayatolee maisha katika Kazi za Kimisionari."  Marehemu Masista hao watatu waliouawa ni Sista  Bernadette Boggian, Sista  Olga Lucia Raschieri  na Sista Lucia Pulici. Inatajwa kwamba , walikuwa wameyatolea maisha yao katika utumishi wa kimisionari barani Afrika.

Katika kumbukumbu ya kupita miaka miwili baada ya mauaji yao licha kwamba bado kuna giza nene juu ya mauaji haya , Alhamis,  Septemba 1, 2016, Shirika la Uchapishaji la EMI,lilichapishaji kitabu hicho  chenye jina "Nenda, kayatolee maisha , katika kazi za kimisionari, kitabu kilicho jumuisha maoni mbalimbali yaliyotolewa na Masista wanashirika wenzao wanaofanya utume wao nchini Burundi na Congo. 








All the contents on this site are copyrighted ©.