Kanisa halihitaji kuwa na utendaji wenye urasimu kama serikali bali kutumikia kwa upendo nahuruma, katika kujali mahitaji ya watu hasa waliosaulika pembezoni katika umaskini na upweke. Ni mawaidha ya Baba Mtakatifu Francikso, aliyoyatoa Jumapili iliyopita mchana kabla ya sala ya Malaika wa Bwana ,mbele ya umati mkubwa wa watu waliofika kumsikiliza, tokea uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican. Papa alionya kwamba, waamini wa Kanisa bila kuwa na mioyo iliyojaa huruma na upendo , kuna hatari kwa kanisa kuwa baridi katika utendaji wake. Alitaja ubaridi huo au imani ya uvuguuvugu tu, maana yake , ni kuw ana utendaji usiyoonyesha dhahiri utambulisho wa kanisa katika maisha ya kijamii.
Maelezo ya Papa, yalinukuu maneno ya Yesu ambamo alisema, "Nimekuja kuleta moto duniani na heri ingekuwa tayari kuna moto mkali”. Papa Francisko alisema, Kristo anataka Roho Mtakatifu kuwasha moto katika mioyo yetu wenye kutufanya kuwa na uwezo wa kutenda kwa upendo na huruma. Moto huu, alielezea, una nguvu katika ubunifu wa kutenda na hutakasa na kumbadili kila mwenye imani kwa Kristo. Ni moto unaochoma kila aina ya mateso ya kibidamu , kila ubinafsi , kila dhambi, hubadilisha mtu toka ndani na kumfanya upya.
Papa aliendelea kufafanua kwamba, , iwapo sisi wenyewe tutajifunua wazi kabisa katika utendaji wa Roho Mtakatifu , tutaweza pata ujasiri na hamasa za kutangaza ujumbe wa Injili wenye kufariji , huruma yake na wokovu kwa kila mtu, ulimwenguni kote, tena kwa uwazi na bila woga. Lakini alionya Papa , moto na hamasa hiyo ni lazima kuanzia ndani ya mioyo yetu.
Alisistiza kwamba kutekeleza lengo la Mungu, Kanisa linahitaji msaada wa Roho Mtakatifu, kwa kuwa ndiye mwenye kuondoa hofu na mashaka yote, na hivyo huweza pata nguvu na ujasiri wa kutembea sehemu zote na katika mipaka yote kwa usalama. Ili kufanikisha hili, hapahitajiki urasimu wa kiserikali kaitka utendaji wake kwa kuwa kufanya hivyo ni kujihatarisha.
Badala yake , aliendelea kuzungumzia ushujaa wa kitume ambao moto wake huwashwa na Roho Mtakatifu ndani ya miaoyo ya watu , moto wenye kusaidia kuvuka kuta na vikwazo, na kuleta ubunifu na nguvu za kusonga mbele katika safari ya maisha ya kuelekea mbinguni , safari ambayo barabara yake imejaa mitego, vishawishi, barabara inayodai kutoa hata sadaka ya maisha kwa ajili ya wengine wote. .
Papa alieleza na kutaja haja ya Mapadre, wote waliowekwa wakfu, na wakristo kwa ujumla , kuwa na hisia hii ya kuwa n hamu ya kuufikia ujumbe wa upendo na huruma kwa watu wote, kwa majirani walio karibu na walio mbali hasa kwa wale walio katika mateso , umasikini na wote wanaoishi katika hali za wasiwasi mwingi kutokana na changamoto za maisha ya kibinadamu , kama wakimbizi .
Papa alieleza hili na kutoa mfano wa Mapadre na watawa wanaume na wanawake, na walei , waliokwenda sehemu mbalimbali za dunia kwa nia ya kutangaza injili kwa upendo mkubwa na uaminifu, wakati mwingine hata kwa gharama ya maisha yao wenyewe. Papa ameutaja kuwa ni ushuhuda unaopaswa kuzingatiwa na kuigwa maana ni mfano unaotukumbusha kwamba, Kanisa halihitaji utendaji wenye urasimu kama serikali bali ni watu wanaotenda kwa huruma toka mioyo mwao ,kuwa wapelekaji wa neno la faraja ambalo ni Yesu mwenyewe kwa watu wote.
Huo ndiyo moto wa Roho Mtakifu. Kama Kanisa halina moto huo na kama haliruhusu moyo huo kuingia ndani mwake, basi Kanisa hilo ni baridi. Liko katika hali ya uvuguvugu tu bila kuwa na uwezo wa kutoa miali ya mwanga wa maisha ya kweli ya Kristo. Hivyo Papa alikamilisha hotuba yake kwa kutoa wito kwa wote kujitafakari iwapo mioyo yao ina uwezo wa kupokea moto huu.
Na aliomba msaada wa maombezi ya Mama Bikira Mari, ili i Moto wa Roho Mtakatifu uweze kuingia katika mioyo ya Wakristo. Na pia alikumbusha Jumapili ilikuwa Sikukuu ya Mtakatifu Maximilian Kolbe, shahidi wa upendo, akisema mfano utakatifu wake, unatufundisha kukumbatia "moto wa upendo kwa Mungu na jirani.
All the contents on this site are copyrighted ©. |